Na Vicky Kimaro, Mwananchi
Dar
es Salaam. “Madaktari waliponiambia kuwa watoto wangu wameungana
nilichanganyikiwa, niliona dunia imenigeuka, sikuwahi kuwaza nitakutana
na kitu cha namna hii katika maisha yangu.”
Ni
maneno ya binti kutoka kabila la Wandali ambalo asili yake ni Mbeya,
Grace Joel (19), ambaye Februari 20 mwaka huu, alijifungua mapacha wa
kiume ambao wameungana katika sehemu ya kiunoni.
Mwanadada
huyo anasema hakuamini macho yake pale madaktari wa Hospitali ya Uyole
iliyopo mkoani humo walipomwambia kuwa watoto wake wameungana na hivyo
kupewa rufaa ya kwenda kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa wa Mbeya.
"Wakati
wa ujauzito wangu sikuwahi hata siku moja kuhisi kuwa ningeweza kuzaa
watoto wakiwa kwenye tatizo hili, sikuwahi kuumwa zaidi ya kuvimba miguu
tu na hiyo ni hali ya kawaida kwa mjamzito yeyote." anasema Grace
ambaye kwa sasa anahitaji msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha ya
watoto wake.
Licha
ya umri huo mdogo, amejikuta kwenye hali ya mateso na uchungu mwingi
baada ya familia yake, hususani mume wake, Erick Mwakyusa kumtelekeza
kwa kile alichodai kuwa hana haja na watoto walioungana.
Kwa msaada ili kuokoa maisha ya
watoto hawa piga namba
Post a Comment