Ajali
imetokea majira ya asubuhi ya leo katika daraja la Mlalakuwa, Mikocheni
jijini Dar ambapo gari hiyo Inayoonekana kuharibika vibaya ilitumbukia
katika mto huo na kusababisha kifo cha Mtu mmoja ambaye anaonekana
akielea juu ya maji.Picha Kwa Hisani ya Kajunason Blog
.Juu na Chini: Picha inayoonesha kipande cha nyama inayodaiwa kuwa ni sehemu ya ubongo wa dereva huyo kikiwa kinanin'ginia katika daraja hilo. chini ni sehemu ya kioo cha mbele kilicho haribiwa vibaya na kubaki na sehemu ya damu
Ajali mbaya na ya kutisha imetokea leo alfajiri katikati ya madaraja mawili ya chuma yaliyoko eneo la Kawe pembeni ya kambi ya JKT Mlalakuwa, Dar es Salaam.
Ajali hiyo imesababisha dereva kupoteza maisha na kuacha vipande vya ubongo vikining’inia katika moja ya madaraja hayo, baada ya gari hilo aina ya Toyota Celica GTR lenye namba za usajili T220ABL kugonga na kisha kuingia kwenye ukingo wa daraja na kisha kutumbukia kwenye mto. Maiti iliondolewa asubuhi wakati ajali hiyo ilitokea kati ya saa 8 na saa 9 alfajiri
Post a Comment