Zanzibar. Rais
wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, amewahimiza wananchi kujitolea
katika kujiletea maendeleo huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea
kuziunga mkono jitihada hizo kwa manufaa yao na Taifa.
Akizungumza katika ufunguzi wa
Kituo cha Afya cha Kajengwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja jana
alisema, Serikali wakati wote itaendelea kuziunga mkono jitihada za
wananchi za kujiletea maendeleo.
Dk Shein aliwaeleza wananchi
waliohudhuria uzinduzi huo ambao ni sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya
Mapinduzi kuwa, uimarishaji wa huduma za afya ni uamuzi uliofanywa na
Chama cha Afro Shirazi kama ulivyobainishwa katika mkutano wake wa
kampeni za uchaguzi Julai 8 ,1964.
Aliwakumbusha wananchi hao
historia ya utoaji huduma za afya kabla ya Mapinduzi ambayo ilikuwa ya
kibaguzi ambapo wananchi wanyonge hawakuweza kupata huduma hizo lakini
hivi sasa jambo hilo limebaki kuwa historia.
Aliwapongeza wananchi hao kwa
kuonyesha moyo wa kujitolea ambapo ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka
1999 hatimaye umekamilika na sasa wanaweza kupata huduma za afya kwa
urahisi.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,
Dk Idrissa Muslim Hija aliishukuru halmashauri hiyo kwa jitihada zake za
kuhakikisha kituo hicho kinakamilika na kuahidi kukitunza.
Katika risala yao iliyosomwa na
Katibu wa Kamati ya Maendeleo, Shehia ya Kajengwa,Nassor Simba Hassan
alisema wananchi hao walieleza kuwa kukamilika kwa kituo hicho
kumewapunguzia tabu ya kufuata huduma hizo mbali.
“Tulipata tabu kufuata huduma
hii masafa marefu na ugumu ulizidi kipindi cha mvua na nyakati za usiku
kwa mama wajawazito na watoto,”ilieleza risala hiyo.
Wakati huo huo Zanzibar imesema
hakuna ushahidi wala uthibitisho wowote uliobaini kwamba Upanga wa
Dhahabu wa Jumuiya ya Jeshi la Polisi la Nchi za Kusini mwa Afrika
(SARPCCO) ulipotelea Zanzibar.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed
ameyasema hayo jana wakati akijibu masuali katika kikao cha baraza la
wawakilishi kinachoendelea huko Chukwani Mjini Unguja.
CHANZO: MWANANCHI
Post a Comment