Mwenyekiti
wa mtaa wa pangani kata ya Makorongoni mjini Iringa Salum Kibaya
akiutazama mwili wa mtoto Raymond Ben Mangungu (2) aliyeuwawa kwa
kukabwa shingo na baba wa kambo wakati wa ugomvi wa kimapenzi kati ya
mwanaume huyo na mama wa mtoto huyo usiku wa leo.
Askari polisi akitazama mwili wa mtoto huyo.
Hali ilivyokutwa ndani ya chumba hicho baada ya tukio.
Wananchi wa Makorongini wakimtazama mwanamke huyo wakati akihojiwa na kaka wa mtuhumiwa wa mauwaji hayo.
Mama
wa mtoto Raymond katikati akimsimulia shemeji yake jinsi ambavyo
mpenzi wake alivyoua mtoto ,kushoto ni mama mzazi wa mwanamke huyo.
Huyu ndie mzazi wa mtoto aliyeuwawa Bi Kudra Kahemela (23)Wanawake wa mtaa wa Pangani Iringa wakiuhifadhi mwili wa mtoto Raymond leo.
KATIKA hali isiyo ya
kawaida mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Pangani kata ya Makorongoni
katika Manispaa ya Iringa Hamis Said maarufu kwa jina la Mwarabu
amemuua kinyama mtoto Raymond Ben Mangungu (2) kutoka na ugomvi wa
kimapenzi kati yake na mama wa mtoto huyo ambae kwake ni mpenzi wake
.
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa
huyo wa mauwaji ya mtoto huyo alikuwa amelewa pombe kupita kiasi
na si mara ya kwanza kulewa kiasi hicho na kutishia kufanya mauwaji
dhidi ya mtoto huyo wa kambo kwa kile alichokuwa akidai kuwa ni fedhea
kwake kuishi na mwanamke ambae ana watoto wawili ambao si damu
yake.
Wakizungumzia juu ya
tukio hilo mashuhuda wa tukio hilo kwa sharti la kutotaja majina yao
walisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa Mwarabu kumpiga mwanamke huyo
na familia yake kwa madai kuwa hataki kuwaona watoto hao wakiendelea
kuishi katika nyumba hiyo ambayo ameipanga yeye .
" Huyu bwana Mwarabu
alikuwa akifanya kazi ya kuuza korosho mitaani na akirudi usiku
amekuwa mkali kwa mwanamke huyo ambae alikuwa akidai kuwa bado
amekuwa na mahusiano na baba wa watoto hao wawili .....hata hivyo
sisi kama majirani tumekuwa tukishindwa kuwaamua kutokana na
mwanaume kuwa na tabia ya kulewa pombe kupita kiasi na hata tukio
hili tulijua ni kawaida yao "
Mtoto Tinito Mangungu (6)
ambae ni kaka na marehemu alisema kuwa baba yao huyo mdogo
alifika usiku na kuwataka wote kuamka kitandani na kuwa hakuna mtu
atakayelala katika chumba hicho kama si damu yake.
"Baba mdogo (Mwarabu)
alirudi usiku akiwa amelewa na kusema hakuna mtu kulala kitandani na
kuanza kumpiga mama kwa meza na viti huku sisi tukilia kumtaka
asimpige mama yetu....baada ya hapo alimchukua mdogo wangu na kuanza
kumkaba shingo na kumwacha kitandani akiwa amelama bila kuamka hadi
sasa mama anasema amekufa"
Akielezea juu ya mkasa
huo uliosababisha mauwaji ya mtoto Raymond mama mzazi wa mtoto huyo
Bi Kudra Kahemela (23) alisema kuwa kwa upande wake baada ya
kutishiwa kuuwawa kwa kipigo alifanikiwa kukimbia katika chumba
hicho na kwenda kujificha nje na baada ya muda mwanaume huyo
alianza kutapika na pale alipoingia kutana kumsaidia ndipo alipopigwa
na kuamua kukimbia kwenda kulala nje ya nyumba hiyo kwa kujiegesha
katika nguzo ya umeme iliyopo nyumba ya pili karibu na nyumba ya
shekhe wa mkoa Juma Alli Tagalile
Alisema kuwa asubuhi
aliingia katika chumba hicho baada ya mwanaume huyo kutoka kwenda
katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Tulivu kuendelea kunywa
pombe na kumkuta mtoto huyo akiwa amelala bila kutikisika .
" Mimi nilijua kama
mtoto amelala tu ama amezimia ila baada ya kuwaita watu wazima
akiwemo mama yangu mzazi ndipo nilipobaini kuwa mtoto wangu Ray
amefariki dunia na ndipo nilipomfuata na kumweleza juu ya tukio
hilo ila bado aliendelea kunywa pombe na kudai kuwa mtoto huyo
amezimia kwa kelele za usiku ."
Alisema baada ya hapo
mwanaume huyo alikimbia hadi Ilala kwa wakwe zake na kuomba msamaha na
kusuluhishwa ugomvi wao ila wakati mtengo wa kukamatwa ukiwekwa
ndipo alipokimbia kusiko julikana.
Mwandishi wa habari hizi
alishuhudia mtoto huyo akiwa amekufa katika kitanda cha wazazi
wake huku chini ya chumba hicho thamani mbali mbali pamoja na vyombo
vikiwa vimevunjika kutokana na ugomvi huo .
Mwenyekiti wa serikali
ya mtaa huo wa Pangani kata ya Makorongini Bw Salum Kibaya
amethibitisha juu ya kifo cha mtoto huyo na kuwa baada ya tukio
hilo ambalo lilitokea usiku wa kuamkia leo jumamosi Desemba 14 mwaka
huu alilazimika kwenda kituo cha polisi cha stendi kuu ya mabasi
yaendeyo mikoani na kuwajulisha juu ya tukio hilo na kufika eneo la
tukio .
Bw Kibaya alithibitisha
pia kuwa ugomvi kati ya wapenzi hao si wa kwanza kutokea japo kwa
maelezo ya mwanamke huyo alikuwa mbioni kuolewa na mwanaume huyo na
hivyo kuwa na wanaume wawili akiwemo mzazi mwenzake ambae kwa sasa
anaishi eneo la Don Bosco mjini hapa.
Mwili wa mtoto huyo
umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa huku jeshi la
polisi likiwahoji mama wa mtoto huyo ,kama wa mtuhumiwa wa mauwaji
hayo ambae ni mkazi wa Mlandizi Kibaha Jijini Dar es Salaam na mama
mzazi wa mtoto aliyepoteza maisha.
CHANZO NI FRANCIS GODWIN
GPL
Post a Comment