Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee
Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15,
2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Dkt Dlamini Zuma kwa
hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa
Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika
Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa
Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za
mapambano ya ukombozi aliyoongoza Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo
ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi
kusini mwa Afrika kwa kuwahifadhi na kuwapa misaada ya hali na mali
wapigania ukombozi wake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni
wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za
mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni
Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia
ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles.Picha na IKULU
Post a Comment