Meneja
mradi wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika
kisiwa cha Kome, Bi. Verdiana Vedastusi, akitoa utangulizi juu ya
misaada hiyo. [picha na Daniel Makaka ,Sengerema] pia chini ni baadhi ya
picha za kukabidhi vifaa hivyo.
Na. Daniel Makaka, Sengerema
SHIRIKA
Lisilo la Kiserikali la Goodneigbours la jijini Mwanza limetoa mahitaji
ya shule na matumizi ya nyumbani kwa watoto mia saba (700) wanaoishi
katika mazingira magumu katika kisiwa cha kome kata ya Nyakasasa
Wilayani Sengerema yenye thamani Tsh 40Millioni.
Akikabidhi
vifaa hivyo Meneja Mradi wa kusaidia watoto hao kupitia shirika hilo,
Bi,Verdiana Vedastu amesema kuwa lengo la kusaidia watoto hao ni
kuwasaidia katika masomo yao na kupata elimu itakaowasaidia katika
maisha yao ya baadaye na kuwa viongozi bora wa kubadilisha kisiwa cha
kome kielimu.
Bi,
Verdiana amevitaja vifaa hivyo kuwa ni kalamu kumi , mifuko ya
madaftari ,sukari kilo mbili, mafuta ya kupikia lita tano,sabuni miche
kumi ya kufuria, vichongeo vya kalamu, lura na unifomu ambapo kila
mtoto alipata mgao wake kati ya watoto mia saba wa vijiji vya Nyakasasa
na kijiji cha Nfunzi.
Ameongeza
kuwa zoezi hilo ni endelevu ambalo litafanyika hadi mwisho wa mradi huo
ambapo ametoa wito kwa jamii hiyo kushirikiana na shirika hilo ili
kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Post a Comment