Watu waliojipanga mitaani wakati mwili ukipelekwa Union Buildings kuagwa siku ya mwisho
Jana
ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa wananchi wa Afrika Kusini na wageni
kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais wa zamani wa taifa hilo Nelson
Mandela, baada ya kutengwa siku tatu kwaajili ya zoezi la kuuaga mwili
wake uliowekwa katika ofisi za serikali jijini Pretoria.
Ripoti
zinasema umati mkubwa ulijitokeza katika siku hizo tatu, na misululu ya
watu wapatao laki moja ilijipanga kwa umbali mrefu wakisubiri kumuaga
shujaa wao jana huku wengine wakiambulia kuuona tu katika gari.
Polisi wakijaribu kuwazuia watu wasiendelee kuingia
Kutokana
na umati mkubwa uliojitokeza, polisi walijaribu kuzuia watu wasiendelee
kuingia kwa kufunga mageti, lakini hata hivyo watu hao walilisukuma na
kutaka kuingia kwa nguvu ili na wao wakatoe heshima zao za mwisho.
Katika vurugu hizo baadhi ya waombolezaji walianguka na kukanyagana, baadhi yao walipata majeraha madogo.
Huko
kijijini Qunu ambako mwili wa Mandela unatarajiwa kupelekwa leo tayari
kwa mazishi yatakayofayika kesho Jumapili, maandalizi yako katika hatua
za mwisho.
Qunu, maandalizi ya mwisho yakifanywa tayari kupokea mwili kwa mazishi kesho
Siku
ya Jumatatu (December 16) baada ya mazishi, Rais wa Afrika Kusini Jacob
Zuma anatarajiwa kuzindua sanamu ya Nelson Mandela, ambayo imeonekana
ikimaliziwa kuwekwa katika ofisi za Serikali ‘Union Buiildings’ jijini
Pretoria jana.
Sanamu ya Mandela ikimaliziwa
Post a Comment