Algeria imefuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia.
The
Desert Foxes walitoka nyuma bao moja kwa nunge dhidi ya Urusi katika
kipindi cha kwanza na kusawazisha na hivyo kufuzu kama mshindi wa pili
katika kundi H nyuma ya UbeljijiHii ndiyo mara yao ya kwanza kupita mkondo wa kwanza.
Algeria
itaingia katika kumbukumbu za historia ya Soka Afrika kuwa mwakilishi wa
6 kuwahi kufuzu kwa raundi hiyo ya 16 bora nyuma ya Cameroon Ghana
Nigeria Morocco na Senegal .
Algeria
ilikuwa imefungwa mapema katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mkwaju
wake Aleksandr Kokorin aliyepata pasi murua kutoka kwa Dmitri Kombarov.
Hata
hivyo vijana wa kocha Fabio Capello walianza kulinda ngome yao mapema
bila ya tahadhari kuwa baop lolote la Algeria ingewarejesha nyumbani.
Mashambulizi
ya Algeria yalizaa matunda kunako dakika ya 60 Islam Slimani
alipoisawazishia Algeria kutokana na mkwaju wa freekick uliopigwa na
Yacine Brahimi.
Wadau
watachunguza tukio ambalo shabiki mmoja anadaiwa kumulika kifaa cha
Laser usoni mwa kipa wa Urusi Igor Akinfeev kabla ya bao hilo la
kusawazisha.
Kocha
Capello amelalamikia hatua ya refarii kupuuza tukio hilo akisema kuwa
huenda marefarii wananjama ya kuihujumu timu ya Urusi.
Urusi
ilifanya mashambulizi kwenye lango la Algeria la Algeria lakini wapi
safu ya ulinzi ilikaa ngangari na kuhimili mashambulizi hadi kipenga cha
mwisho na hivyo kuipa Algeria alama moja muhimu iliyoiwezesha kuweka
historia ya kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia.
Algeria sasa imeratibiwa kukwaruzana na Ujerumani katika mechi ya 16 bora siku ya jumatatu.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment