Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lowassa atoa siku saba kwa H/Monduli

Monduli. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameipa wiki moja Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kuzipatia ardhi kaya 63 za Kijiji cha Nanja, ambazo zimetakiwa kupisha eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani hapa.
              
Akizungumza katika uzinduzi wa Bwawa la Migwara lililojengwa upya na kampuni ya Ms Meero Contractors kwa thamani ya Sh870.1 milioni. Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, alisema wananchi hao wanapaswa kuhamishiwa katika shamba lililokuwa la mwekezaji la Oguru ambalo sasa linamilikiwa na halmashauri.


Alisema sambamba na mifugo yao, wanapaswa kuhamia katika eneo hilo kabla ya mwezi huu, kwani tayari Halmashauri ya Monduli ilishafanya uamuzi wa kuwapa ardhi hiyo zaidi ya miaka miwili iliyopita, lakini suala hilo halijatekelezwa.

“Halmashauri ya Monduli ina madiwani wengi vijana, lakini cha ajabu wanafanya kazi taratibu kama konokono. Tukifanya uamuzi inachukua muda mrefu kutekelezwa, tulishaamua Shamba la Oguru litakaliwa na familia 63 za Nanja na mifugo yao,” alisema Lowassa.

Alisema wakati halmashauri hiyo ikiwa inatekeleza mpango wa kuwanyang’anya wawekezaji mashamba 43 waliyoyatelekeza, yale ambayo tayari yapo mikononi mwa halmashauri wayagawe kwa wananchi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top