Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MASKINI WATOTO HAWA .... WAFA KWA KULIPULIWA NA PETROL ... SOMA HAPA UJUE KISA KAMILI

 


Haruni Sanchawa na Roda Josiah, Bagamoyo
WATOTO wawili wa familia moja, Nuru (3) na Dora  Kaitaba (2), wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kubaki majivu baada ya moto mkubwa uliotokana na petroli kulipuka nyumbani kwao, Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mtoto Dora Kaitaba (2) wakati wa uhai wake.
Tukio hilo lililowaliza wengi, lilijiri saa tatu usiku, Jumapili iliyopita watoto hao wakiwa ndani na baba yao.
Kwa mujibu wa mashuhuda, baba mzazi wa watoto hao, Kaitaba ambaye ni mpiga picha wa kujitegemea, alikuwa amerejea kutoka Bunju B alikofuata petroli ambayo huiuza katika vipimo vidogo vya kwenye makopo ya maji nyumbani hapo.

Ilizidi kudaiwa kuwa alipofika kwake alishusha mzigo wa mafuta, watoto wake hao walikuwa wamelala katika kibanda chake cha biashara.
Mtoto Nuru Kaitaba (3) enzi za uhai wake.


Ghafla, mashuhuda wanasema, umeme ulikatika hali iliyomfanya Kaitaba kuchukua mshumaa na kuuwasha ili andelee na shughuli zake za kuhudumia wateja.
“Baada ya kuwasha mshumaa, moto huo ulidakwa na petroli hiyo iliyokuwa kwenye dumu na kusababisha mlipuko mkubwa.

Mama mzazi wa wa watoto hao (aliyenyosha mikono) akiwa na simanzi kwa kuwapoteza wanaye.
Mashuhuda walisema Kaitaba alikimbia kutoka bandani, lakini alipopata akili ya kuwaokoa watoto wake tayari moto ulishakuwa mkubwa na hivyo kumfanya apige kelele za kuomba msaada.
Mchungaji akiziombea roho za marehemu hao, zikapate kupumzika kwa amani.
Hata hivyo, majirani walishindwa kuingia ndani kutokana na ukubwa wa moto huo na uduni wa vifaa vya kuzimia.
Watu wakiwa wanaangalia tukio hilo kwa masikitiko makubwa, Kikosi cha Zimamoto Bagamoyo kiliwasili kikiwa kimechelewa hivyo kuambulia kuchukua majivu ya watoto hao wawili waliaochana mwaka mmoja kuzaliwa.

...Ndugu na jamaa wa karibu wakiwaaga watoto hao.
Kamanda  wa Polisi  Mkoa wa  Pwani, SACP Onesphory Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tofauti na madai ya baadhi ya watu kuwa baba mzazi wa watoto hao anashikiliwa na polisi, alichukuliwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kutibiwa majeraha na hatachukuliwa hatua yoyote kwa vile kilichotokea ni ajali.
Aidha Kamanda Matei alitumia fursa hiyo kupiga marufuku biashara hiyo ya mafuta ya petroli na dizeli ambayo ni maarufu wilayani humo.

Wakinamama wakipanda gari kuelekea kwenye mazishi ya watoto Nuru na Dora.
Marehemu walizikwa Jumatatu iliyopita kwenye Makaburi ya Bunju, Kinondoni, Dar.
 Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

GPL
Download Our App

1 comments:

ninawapa pole wazazi na ndugu wa marehemu mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi amina

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top