Wewe unadhani ukatili wa kijinsia ni kwa wazazi au walezi tu kwenda
kwa watoto? Hapana hata kwa baadhi ya wazazi pia inatokea kwa kufanyiwa
ukatili na watoto wao ila hushindwa kujitokeza hadharani kusema mbele ya
jamii kwa aibu au kufanya hivyo mara chache.
Hii imemtokea mwanamke huyu aitwaye Bobbi kutoka Southampton ,
Uingereza ambapo anasimulia jinsi alivyofanyiwa ukatili na mtoto wake
mwenye umri wa miaka tisa akitaka kumchoma kisu na wakati mwingine
kumvizia akitaka kumuua.
Mtoto huyo aitwaye JJ mara kadhaa amekuwa akifanya mashambulizi ya
vurugu kwa mama yake kwa kumpiga, kumrushia vitu kichwani na wakati
mwingine kumvuta nywele ambapo katika tukio jingine alijaribu kumchoma
kisu akitaka kumuua.
Hali hiyo ilimlazimu Bobbi kuondoa vitu vyote vyenye ncha kali karibu
na nyumbani ili kuepusha hatari ambapo hata kwa baba yake wa kambo
imekuwa ngumu kwake kuishi pamoja na mtoto huyo kwani ni vita kali.
Post a Comment