Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polisi waanza uchunguzi matapeli wa meseji za simu


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kimesema kuwa kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwa nia ya kuwatapeli wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao makuu, Barnabas Mwakalukwa, leo imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa katika kituo cha polisi alichokaribu nacho.

“Tunawataka wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au ‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata wateja wengi... sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto na nyingine kama hizo.’

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kutumia mitandao pamoja na simu katika kuelimisha na kuhabarisha na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi kupuuzia  jumbe hizo zenye lengo la kitapeli.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top