Na
Mwandishi wetu
WAWAKILISHI
wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani wataendesha semina kwa
wadau wa michezo hapa nchini katika
ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
Wawakilishi
hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu ambaye kwa sasa ni
mtangazaji , Kasey Keller .
Wakiwa
nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania
Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao utangazwa hapo
baadaye.
Ziara hiyo ni moja ya kukuza
ushirikiano baina ya Seattle Sounders na wadau wa michezo nchini na
ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho
Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester
United.
Kwa
kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA), wawakilsihi wa timu hiyo
pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha ikiwa pamoja na World
Vision, taasisu ya PATH na Chuo kijulikanacho
kwa jina la Washington State University's Paul G. Allen School for Global
Animal.
"Ziara hii itadumisha na
kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa timu
hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi wakubwa wa
timu yao katika ziara hiyo.
Alisema
kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na
jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika
ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la kushughulika na masuala
ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.
Post a Comment