Mkurugenzi wa Mad Mad Entertainment, Yasmin
Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania
watakaokwenda Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya
kutengeneza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior,
Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon
Mwakifamba.
Msanii wa filamu, Steve Nyerere
(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania, Simon Mwakifamba.
*****
KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment iliyopo
jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya kupeleka wasanii wa
filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza sanaa hiyo hapa
nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak
alisema ameamua kufanya kazi na wasanii hao ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua
kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.
“Kwa
muda mrefu niliokaa London sioni kama sanaa hii ina
maendeleo, nikafikiria kitu gani
nifanye ili kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa
nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo
kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa
hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya
kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na
wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa
vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema
Razak.
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua
vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu
kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo
katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalienamna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.
Post a Comment