Mchezaji wa timu ya waendesha Bodaboda kutoka Tegeta akiwania mpira
mbele ya mchezaji wa timu ya Waendesha Bodaboda kutoka Kawe katika
mashindano ya ligi ya Bodaboda Cup inayoendeshwa na Jeshi la polisi
kikosi cha usalama barabarani ambapo timu ya Kawe imeifunga timu ya
Tegeta kwa magoli 3-0 kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa
Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam leo.
Mashindano hayo yanashirikisha
timu mkoa wa kipolizi wa Kinondoni ambazo zinatoka katika maeneo ya
Kimara, Kawe, Tegeta, Mabibo na Ubungo wachezaji wakiwa ni waendesha
Booda, awamu ya kwanza ya ligi hiyo ilikuwa na timu 32 na sasa ni awamu
ya pili ambapo timu 16 zinashindana ili kupata timu 8 zitakazoshiriki
Ligi ya Nane Bora na hatimaye kupata mshindi wa mashindano hayo ya
Kinondoni Bodaboda Cup ambaye atapata zawadi nono.
Lengo la Mashindano hayo ni
kuwakutanisha waendesha Bodaboda wote wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni
ili waweze kufahamiana wao kwa wao, lakini pia ili jeshi la polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani liweze kuwaelimisha juu ya sheria za
usalama Barabarani na Ulinzi Shirikishi kwa jamii.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Agatha Isack akikagua timu kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye
uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Agatha Isack akikagua timu kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye
uwanja wa Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani
Agatha Isack akimtakia uchezeshaji mwema mshika kibendera wa kushoto
Hamis Pondamali kabla ya kuanza kwa michezo hiyo leo kwenye uwanja wa
Tanganyika Pakers jijini Dar es salaam.
Timu ya Kawe ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo na kupata mawaidha mawili matatu.
Kikosi cha timu ya Tegeta kikiwa katika picha ya pamoja kalba ya kuanza
kwa mchezo huo timu hiyo imefungwa magoli 3-0 na timu ya Kawe.
Wachezaji
wa timu za Kawe na Tegeta wakiwania mpira uliojuu wakati wa mchezo
uliokutanisha timu hizo leo kwenye uwanja wa Tanganyika PakersKawe
jijini Dar es salaam
Kutoka
kulia ni Aghata Isack Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani, Esther Ngaja Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani, Refarii wa mchezo huo Geofrey Mwamboneke,
Mshika Kibendera Hamis Pondamali, Mshika Kibendera Mwanahamisi Matiku,
ASP. Emilian Kamuhanda Insp.Soud Ramadhan na Mratibu wa kombe hilo
Ernest Mbaga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa
mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers leo,
Post a Comment