Na
Fadhili Athumani, Kilimanjaro
WAREMBO 12 wanaotarajiwa kupanda jukwaani Juni 15 mwaka huu kuchuana katika shindano la kumsaka malkia wa urembo mkoani Kilimanjaro, Redds Miss Kilimanjaro 2013 wameingia kambini leo.
Redds Miss Kilimanjaro 2013 inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original, Panone and Company Ltd, Bonite Bottlers kupitia kinywaji baridi cha Cocacola na maji ya Kilimanjaro, Mr. Price, Hugo Hotel na Kilimanjaro Express Bus.
WAREMBO 12 wanaotarajiwa kupanda jukwaani Juni 15 mwaka huu kuchuana katika shindano la kumsaka malkia wa urembo mkoani Kilimanjaro, Redds Miss Kilimanjaro 2013 wameingia kambini leo.
Baadhi ya washiriki wa Miss Kilimanjaro
2013
Walimbwende hao wanaotarajia kupambana kumpata
Mrithi wa Redds Miss Kilimanjaro 2012, Anande Michael anayeshikilia taji hilo
kwa sasa, wameweka kambi katika hoteli ya Hugo, iliyoko nje kidogo ya mji wa
Moshi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa
Mashindano hayo, Mkurugenzi wa Kampuni wa Rick Plan Company Ltd, Jackline Chuwa
alisema ameamua kuwaingiza warembo kambini mapema ili kuhakikisha kuwa
mashindano ya mwaka huu yanakuwa tofauti na ya mwaka
jana.
“Warembo wanaingia kambini Le,
ili kuhakikisha kuwa mashindano yanakuwa ya kipekee, tuimeboresha
mamnbo mengio na lengo ni kumpata Redds Miss Tanzania 2013, warembo wapo pale
Hugo Hotel,” alisema Chuwa.
Mkurugenzi huyo alisema mashindano ya mwaka
huu yatafanyika Juni 15 mwaka huu, kuanzia saa moja kamili jioni katikia ukumbi
wa La Liga Carnivore na kuongeza kuwa viingilio ni sh. 15,000 kwa viti vya
kawaida n ash. 30,000 kwa viti vya watu maalum (VIP).
Kuhusu Burudani, Mkurugenzi huyo aliwataja
wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na JB, msanii wa kimataifa kutoka Burundi,
Kidumu na Bendi yake, Ngoma za asili na Sarakasi huku mgeni Rasmi akitarajiwa
kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Post a Comment