Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUJIUNGA NA CCM

E83A0580 0081fMjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) manispaa ya Singida, Hassan Mazala akizungumza juzi kwenye halfa ya uzinduzi wa hotel ya ya Chemuchemu park na shina la wakereketwa wa CCM wa hoteli hiyo mpya.
                                                                            *******
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida Hassan Mazala, amewahimiza wafanyabiashara wa ngazi zote kujiunga na CCM, kwa madai kuwa ni chama pekee kinachowajengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu.
Mazala ametoa wito huo muda mfupi baada ya kuzindua tawi la wakereketwa wa hotel mpya na ya kisasa ya Chemuchemu Park, iliyopo katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wafanyabiashara wamekuwa wakishirikiana na CCM kwa muda mrefu na hali hiyo inapaswa kuendelezwa kwa sababu inazinufaisha pande zote mbili.
Akifafanua zaidi amesema amani na utulivu ndio inayopelekea wafanyabiashara na Watanzania wengine wote, wafanye shughuli zao halali kwa uhuru mpana zaidi na ambao hauathiri sheria zilizowekwa.
MNEC huyo amesema CHADEMA inaonyesha ilani yake ni kupandikiza chuki, hasira, kuchonganisha watu na upotoshaji uliopitiliza, na kwa hali hiyo, CHADEMA sio mahali rafiki kwa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mazala ametumia fursa hiyo kuwahimiza viongozi/watendaji wa CCM na wa serikali yake, kuwa karibu na wafanyabiashara ili kujua matatizo/kero wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kwa upande wa wafanyabiashara, amewataka wafanye kazi halali kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa na kuhakikisha wanabana matumizi au wawe na nidhamu ya matumizi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top