MGOGORO wa kisiasa visiwani Zanzibar umeendelea kuchukua sura mpya baada ya Baraza la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) wilaya ya Sumbawanga mjini katika mkoa wa Rukwa kutoa tamko la kuunga mkono uamuzi wa chama cha wananchi CUF kutokubaliana na maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.
Wajumbe wa BAWACHA Sumbawanga mjini wametoa tamko hilo katika kikao cha Baraza cha kwanza kwa mwaka 2016 kilichofanyika katika ukumbi wa CWT mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga na kuweka msimamo wa kuunga mkono uamuzi wa Chama cha wananchi CUF kukataa uchaguzi wa marudio na kuwaomba wanawake nchini kuungana katika maombi.
Tamko hilo limetolewa na mbunge wa viti maalumu mkoa wa rukwa kwa tiketi ya Chadema ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la vijana mkoa wa Rukwa, Mhe. AIDA JOSEPH na kuungwa mkono na Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Rukwa, Honoratha Wamayi.
Mkutano mkuu wa Baraza la wanawake wa CHADEMA wilaya ya Sumbawanga umefanya mgawanyo wa kazi kwa madiwani wa viti maalumu kwa kila kata ili kuwaunganisha wanawake wa wilaya hiyo na kuwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
Kwa Undani4 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment