Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA MSIKITINJ JIJINI MWANZA



Mnamo tarehe 18.05.2016 majira ya saa 20:30hrs katika msikiti wa Masjid Rahman uliopo Ibanda Relini mtaa wa Utemini @ mapankini kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana jiji na mkoa wa Mwanza. 




Watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga, shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla katika msikiti tajwa hapo juu wakati waumini wa msikiti huo wakiwa wanaswali na kuzima taa na kutoa sauti wakisema “kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi ?” na hapo hapo wakaanza kuwakata kwa mapanga baadhi ya waumini katika sehemu mbalimbali za miili yao. 




Walipata majeraha makubwa kichwani, shingoni na mikononi na walipoteza maisha yao papo hapo na mmoja kupata majeraha sehemu za kichwani na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Nyamagana (Butimba). 



Waliouawa, 1. Feruz ismail elias mika 27, muha Imamu wa msikiti huo na mkazi wa Ibanda relini, 2. Mbwana Rajab miaka 40, Mbondei mfanyabiashara na mkazi wa ibanda, 3. Khamisi mponda miaka 28 dereva wa kiwanda cha samaki (TFP), mkazi wa Mkolani, wote walijeruhiwa sehemu za kichwani, shingoni na mikononi. 




Aliyejeruhiwa ni Ismail Abeid @ Ghati miaka 13, mkurya mwanafunzi wa madrasa katika shule ya kiislamu itwayo Jabar hila iliyoko maeneo ya Nyasaka aliyepata majeraha kichwani na anapata matibabu hospitali ya Nyamagana. 



Kutokana na hali hiyo, waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wakipiga mayowe yaliyopelekea wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti chupa mbili za konyagi zilizokuwa na petroli na tambi za moto, chupa moja ililipuka lakini haikuleta madhara makubwa. 


Jeshila la polisi limewakamata washukiwa watatu kwa ajili ya kuwahoji kuhusiana na tukio hilo, huku msako mkali wa kuwasaka watu wengine walio husika kwa namna moja au nyingine kwenye mauaji hayo ukiwa bado unaendelea. 


Napenda kuwaeleza wananchi watulie wakati tukiendelea na upelelezi wa tukio hili, na natoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu wa mauaji hayo ili tuweze kuwakamata. 


Pia nashauri na kusisitiza kuwepo na kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada, kumbi za starehe pamoja na mitaa yao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo. 


Imesainiwa na: 
………………………. 
Sacp: Ahmed Msangi 
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top