Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
JESHI la Polisi nchini kwa
kushirikiana na Mamlaka mapato nchini (TRA) limeboresha mfumo wa utoaji leseni
za udereva ambazo zimeanza kutolewa kwa njia aya Smart Card ili kuendana na
ukuaji wa Teknolojia duniani.
Wakizungumza na wandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Mnadhimu wa kikosi cha usalama barabarani ACP Johandani Kahatano na
Naibu Kamishna wa TRA Yusuph Salum wamesema kuwa mwisho wa kubadilisha leseni
kwa maedeleva wote ni Machi 31 Mwaka huu.
Wameeleza kuwa baada ya muda huo zoezi la
ubadilishaji Leseni za aina zote halitafanyika na mfumo wa utoaji Leseni
utabadilishwa ili kubakia na uwezo wa kutoa Lesseni kwa madereva wanaoomba
Lesseni kwa mara ya kwanza.
Hivyo madereva wote wametakiwa kuhakikisha
wanatumia muda huo wa miezi mitatu iliyotolewa kubadilisha Leseni zao ili
kujiepusha na usumbufu unaoweza kuwapata.
Aidha Kamanda Kahatano amesema kuwa Dereva
atakayekutwa anaendesha gari wakati leseni yake imekwisha atafikishwa mahakamani
pamoja na mmiliki wa gari hilo.
Zoezi la kutoa leseni mpya za udereva
lilianza Oktoba Mosi Mwaka 2010 kwa awamu ya kwanza iliyohusisha mikoa (9) na
machi 2011 mikoa mingine 13 ilianza kutoa leseni hivyo zoezi hilo
kukamilika.
Kamanda huyo amesema kuwa madhumini ya zoezi
hilo ni kubadili mfumo huo na kuondoa tatizo la kughushi pamoja na kudhibiti
mienendo ya madreva kwa kutunza kumbukumbuku za makosa
yao.
Hadi kufikia Disemba 31 Mwaka jana leseni
616,349 zilizokuwa zimetolewa kwa nchi nzima ambapo kati ya hizo leseni 135721
ni za kundi lenye madaraja C zingine 480,628 ni za makundi
mengine.
Hata hivyo takwimu hizo zikilinganishwa na
idadi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa na Mamlaka ya TRA nchini hadi kufikia
Disemba 2012 vinafikia 1,164,574 hiyo inaoonyesha kuwa kuna madereva
wanaoendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na leseni
halali.
Post a Comment