Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.

Wameyasema hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.

Amesema huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.

“Kwa mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa.

Naye Richard Mgulumu Diwani wa kata ya Mlali ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vituo vya afya nchini, hasa kituo cha afya cha Mlali ambapo anasema kuwa awali kituo hicho kilikuwa na wodi chache ambazo zilikuwa hazitoshi kuhudumia wananchi lakini kwa sasa zimeongezeka jambo ambalo litasaidia kuondoa kero za utoaji wa Huduma za afya katika Halamashauri hiyo.

Amesema kuwa Kituo hicho cha afya kimekuwa kikipata wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya Kiteto, Wialaya ya Mpwapwa na Malali hivyo kwa ujenzi huo kutasaidia kuwahudumia wananchi maskini ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma bora za afya.

Naye Mganga Mkuu Hospitali ya Jiji la Dodoma Dkt. James Kiologwe ameipongeza Kamati ya Ujenzi ya kituo cha afya cha Mlali kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho na kuonyesha uzalendo wa kusaidia jamii.
Aidha timu ya Ufuatiliaji wa ujenzi wa vituo vya afya Jijini Dodoma imekagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Mlali, Chamwino, Hombolo na Makole.
 
Majengo ya Upasuaji na wodi ya Wazazi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Mlali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu      ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo

Diamond Aungana na familia Yake kwa Mara ya Kwanza Tangu Alipogombana na Mama Watoto Wake.

Baaada ya tetesi nyingi kusambaa kwamba mwanamuziki Diamond Platinumz inawezekana amerudiana na mama mzazi wa watoto wake Zari the bossy ambae kwa sasa yuko Afrika ya Kusini, sasa imethibitika baada ya kusambaa kwa picha ikimuonyesha msanii huyo akiwa na watoto wake.

Pamoja na kwamba mara ya kwanza alikuwa akisema amekuwa akienda kuwaona watoto wake afrika ya kusini lakini hakukuwahi kuwa na picha iliyowahi kuthibitisha  hilo mpaka jana walipotoa picha hiyo kwa mara ya kwanza kwa takribani miezi minne tangu walipokuwa wamegombana

Naibu Spika Amkingia Kifua Waziri Mkuu Kuujibia Waraka Wa KKKT


Siku moja baada ya Msajili wa Vyama kuiandikia barua Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  kukanusha waraka walioutoa wakati wa Pasaka, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ameitaka Serikali kutoa kauli kuhusiana na hilo.

Mbatia ameihoji serikali leo wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, jana msajili wa vyama ameiandikia kanisa la KKKT barua akitaka ifute waraka wake wa pasaka, serikali inatoa kauli gani kuhusiana hilo na ikizingatiwa hawa ni wadau wakubwa wa amani kwa taifa letu na hapo spika ameanza kwa kuomba dua,”amehoji Mbatia.

Kutokana na hilo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amemkia kifua Waziri Mkuu akisema kwamba itakumbukwa kuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alihoji kuhusu masuala ya dini lakini Spika Job Ndugai akamwambia waziri mkuu hawezi kujibu masuala ya imani.

“Mtakumbuka kuwa Kubenea aliwahi kuuliza masuala ya dini hapa lakini spika akamwambia kwamba waziri mkuu hawezi kujibu swali hilo kwa kuwa ni suala la imani,”amesema.

Waziri Mkuu: Kutangaza Nyongeza Ya Mishahara Hadharani Kuna Madhara


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi kuwa suala la kutangaza nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma hadharani husababisha athari kwa jamii nzima na kwa wale ambao siyo watumishi.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwa bungeni kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge Suzani Lyimo aliyehoji ni kwa nini serikali ya awamu ya tano inakiuka sheria ya utumishi wa umma ya kutoa nyongeza kwa watumishi wake.

Mh. Majaliwa amesema kwamba siyo kwamba serikali haikusudii kuongeza mshahara kwa watumishi wake  lakini kutumia siku kama Mei 1 kutangaza nyongeza za mishahara husababisha athari kwa wananchi wote kwani vitu vinaweza kupanda bei na kusababisha usumbufu kwa watu wengine wasiopokea mishahara.

Pamoja na hayo, Mh Majaliwa ameeleza kuwa "Suala la mshahara ni siri ya mtu. Siyo lazima litangazwe hadharani. Ndiyo maana hata tunapolipa madeni hatutangazi lakini wanaodai wanaona kwenye mishahara yao kwamba malipo yanaingia. Lengo la serikali ni kupunguza na gharama za maisha".

Ameongeza "Serikali ina utaratibu wa kuwapa stahiki watumishi kadiri inavyotakiwa na inaratibiwa vizuri.  Tunaendelea na uboreshaji wa maeneo hayo kama nyongeza za mshahara, na upandishaji wa wa madaja. Watumishi wawe na imani na serikali. Rais alitenga zaidi ya bilioni 200 na tumeshaanza kulipa madeni. Nyongeza za mishahara zitatolewa kwani Rais alikwisha ahidi"

TANZIA: Msanii wa Bongo Fleva Sam wa ukweli afariki Dunia

 
Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Chanzo cha kifo chake kimelelezwa na Producer wake Steve kuwa “Sam alianza kuzidiwa toka J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema ukimwi lakini sio ukimwi wa kawaida bali wa kulogwa”

Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa.

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Athumani Selemani Mbuttuka  kuwa wa Msajili wa Hazina.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa. Mbuttuka utaanza  Juni 6, 2018.

Aidha, kabla ya uteuzi huo, Mbuttuka alikuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Taifa (DAG) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali  (NAOT).

Mbuttuka anachukua nafasi ya Dkt. Oswald Mashindano ambaye tayari amekwisha staaafu.


Waziri Ndalichako : “Maria na Consolata ni Mashujaa wa Taifa”



 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameongoza waombolezaji  kutoa heshima za mwisho kwa Mapacha walioungana Maria na Consolata mkoani Iringa amabapo alizungumza na waandishi wa habari na kusema mapacha hao  Maria na Consolata  ni  mashujaa wa Taifa  na kwamba wameliacha taifa katika simanzi nzito.

"Mara ya mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.

Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo.

Rais Magufuli Atuma Salamu Za Rambirambi Kufuatia Vifo Katika Ajali Mkoani Kigoma





Polisi waanza uchunguzi matapeli wa meseji za simu


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kimesema kuwa kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwa nia ya kuwatapeli wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao makuu, Barnabas Mwakalukwa, leo imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa katika kituo cha polisi alichokaribu nacho.

“Tunawataka wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au ‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata wateja wengi... sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto na nyingine kama hizo.’

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kutumia mitandao pamoja na simu katika kuelimisha na kuhabarisha na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi kupuuzia  jumbe hizo zenye lengo la kitapeli.

Serikali Yalitaka Baraza la Maaskofu KKKT Kuufuta Waraka wa Pasaka


Serikali  ya Tanzania imelitaka Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Tanzania kufuta waraka lililoutoa wakati wa mfungo wa kwaresma kwa madai kuwa Baraza hilo halina mamlaka kisheria ya kutoa waraka huo.

Leo Juni 6, 2018 imesambazwa barua inayoonyesha imeandikwa na Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa mwenyekiti /askofu mkuu wa KKKT iliyoandikwa Mei 30, 2018 ikitoa maelekezo ya kufutwa waraka huo ndani ya siku 10 tangu ilipoandikwa barua hiyo.

Ikiwa na kichwa cha habari ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa KKKT’ barua hiyo inaeleza baraza hilo halitambuliki kisheria katika ofisi ya msajili.


Aidha, barua hiyo inaeleza kuwa Katiba inayotumiwa na Kanisa hilo ni ya mwaka 1960 ambayo ilipitishwa na msajili mwaka 1963. Hivyo Serikali inalitaka Kanisa hilo kuomba kibali cha kufanya marekebisho ya katiba hiyo.

==>Bado tunaendelea kufuatilia uhalisia wa barua hiyo ambayo iko hapo chini  na tutaendelea kukujuza.


Serikali Yatangaza Neema ya Ajira kwa Wataalamu Sekta Ya Umwagiliaji


Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatarajia kuwaajiri wataalamu wa kutosha katika fani ya umwagiliaji.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Waziri wa wizara hiyo, Isaac Kamwelwe wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Shally Raymond ambaye alihoji iwapo kuna mpango wowote unaotekelezwa wa kuwapata wataalamu wa umwagiliaji katika muda mfupi.

Akijibu swali hilo, Kamwelwe amesema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kufanya mawasiliano na Ofisi ya Rais- Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kupata kibali cha kuajiri wataalamu wa kutosha katika fani ya umwagiliaji.

“Pamoja na hayo halmashauri ambazo hazina wataalam wa umwagiliaji zinashauriwa kuajiri watalaamu wa fani hizo,” amesema.

Kauli ya Serikali Kuhusu Milioni 50 Kwa Kila Kijiji


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji itaanza kutekelezwa mara baada ya mfumo wa kuanza kuzitoa utakapokamilika.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo jana jioni bungeni wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa aliyoitoa wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati kupitia vifungu kwa vifungu vya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19.

Bashungwa alisema, “Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020, tulitoa ahadi ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji.” “Bajeti ya mwaka 2016/17 ilitengwa Sh60 bilioni na mwaka 2017/18 ilitenga Sh60 bilioni lakini mpaka sasa hazijaenda, nataka kujua kwa nini hazijaenda?”

Akijibu hoja hiyo, Dk Mpango alisema, “ni kweli jambo hili ni ahadi ya chama na ninaomba nikumbushe kwamba ni ahadi ya chama kwa kipindi cha miaka mitano.

Waziri Mkuu Atoa Ujumbe Mzito Kwa Wabunge


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wabunge kuonyesha mshikamano na kupendana ili waendeleze jukumu la kuishauri Serikali.

Kiongozi huyo wa Serikali alitoa kauli hiyo jana  katika futari aliyoiandaa kwa wabunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge.

“Nasisitiza mshikamano miongoni mwetu katika Bunge hili la Bajeti tangu lianze, tumeonyesha mshikamano na tuendeleze mshikamano huu na kupendana miongoni mwetu ili tuendelee na jukumu la kuishauri serikali,” alisema Majaliwa.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa shukrani kwa niaba ya wabunge alisema ni heshima kubwa kwani kualikwa na Waziri Mkuu si jambo ndogo.

“Kwa hiyo tujihesabie katika waliobahatika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunakushukuru na tunakuombea Mwenyezi Mungu akuongezee pale palipopungua,” alisema Spika Ndugai.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, imehudhuriwa na wabunge karibu wote wakiwamo wa upinzani.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA TZ NA NJE JUNI 7, 2018

         




















































Polepole Awafungukia Mbowe na Zitto Kabwe Baada ya Kutangaza Kuungana

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Ndg. Humphrey Polepole amewaonya Vongozi wa vyama vya Upinzani nchini, Mbowe pamoja na Zitto Kabwe baada ya kukubaliana kushirikiana kumpata Mbunge jimbo la Buyungu lililoachwa wazi na Mwl. Kasuku Bilago kwa kuwaambia wembe wa CCM ni ule ule.

Polepole amesema hayo ikiwa zimepita siku kadhaa baada ya mazishi ya Mwl. Kasuku Bilago kuzikwa huko Kakonko mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kisha kwenda kuzikwa huko kijijini kwao.

Polepole amesema kuwa "Nimesikia jamaa palepale msibani walianza kugawana ubunge na kuanza kujihadaa, ni bahati mbaya sana. Utamaduni wa kiafrika ni kumaliza msiba ambapo lengo ni kufariji wafiwa".

Ameongeza kuwa "Nimekaa Kakonko kwa muda wa kutosha, kwakuwa mmeanza siasa msibani, CCM tunasema wembe ni uleule".

Wakiwa kwenye mazishi ya Mwalimu Bilago ambaye alikuwa Mbunge kupitia CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Mbowe walikubaliana kuweka umoja ambao utamsimamisha mgombea mmoja anayekubalika kutoka upinzani na kuhakikishia wanampigania hadi anashinda ili kumuenzi mwalimu

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top