Mama mmoja mwenye umri wa miaka 33 Sara Ege (pichani kushoto) amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumpiga hadi kumuua mwanae wa kiume kwa kushindwa kuhifadhi mafundisho ya Koran, na kisha kuuchoma mwili wa mtoto huyo kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Mama huyo alianguka pindi hukumu hiyo iliposomwa katika mahakama ya Cardiff Crown hivyo kulazimika kusaidiwa na watu huku akitetemeka na kuangua kilio.
Mahakama iliambiwa kuwa mama huyo alikuwa akimtesa na kumfanya mtoto Yaseen (pichani kulia) kama mbwa, akimpiga kwa fimbo mara kwa mara akimtuhumu kushindwa kukumbuka haraka mafundisho ya kwenye Koran.
Ege amekutwa na makosa ya mauaji na pia kutaka kupotosha ukweli wa sheria
Post a Comment