Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KENYA KUWAMALIZA WAKULIMA WA TANZANIA

 BAADA ya kupokea taarifa za ugonjwa mpya wa mahindi  kutokea Kenya, Serikali imewataka wadau wote wa kilimo kuhakikisha mbegu hizo kabla hazijaingizwa nchini, sampuli nilazima ichukuliwe na kupelekwa kituo cha karantini cha ‘Tropical Pesticide Research Institute, (TPRI), kilichopo  Arusha kwa ajiri ya kuzihakiki ili kuthibiti ugonjwa huo kuingia nchini.   
  Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mohamed Muya, ilieleza kuwa wamepokea taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na Shirika la Kilimo na Chakula (Food and Agriculture Organization), juu ya kuwepo ugonjwa huo wa mahindi unaojulikana kwa jina la ‘Maize Lethal Necrotic Disease (MLND)’ ambapo  ugonjwa huo unasababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalamu “Maize Chlorotic Mottle Virus (MCMV)” na “Sugarcane Mosaic Virus (SCMV)”.
 Alisema , ugonjwa huo ulianzia katika eneo la Bomet lililopo katika Bonde la Ufa ambapo ulisababisha asilimia 100 ya uharibifu wa zao la mahindi lililokuwepo shambani. 
 Muya alisema kulingana na taarifa hiyo, hadi sasa ugonjwa huo umesambaa katika eneo kubwa ndani ya bonde la ufa na umeenea  katika wilaya 22 ambapo jumla ya hekta 16,000 za zao la mahindi zimeathirika ambapo hasara kutokana na ugonjwa huo inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 60 hadi 90.
 Alibainisha kuwa Ili kukabiliana na hatari ya uwezekano wa ugonjwa huo kuingia nchini Tanzania, Wizara inawaarifu wadau wote wa kilimo nchini kuzingatia maelekezo kutoka kwa wataalam.
 Muya alisema kwa kuwa ugonjwa huo unaenezwa na mbegu, Tanzania inaagiza kiasi kikubwa cha mbegu kutoka nje ya nchi, vibali vyote vinavyotolewa kuingiza mbegu hizo lazima ziwe hazina vimelea vya “Maize Lethal Necrotic Disease’ baada ya  kufanyika kwa uchunguzi wa maabara.
 
Aidha, Halmashauri za Wilaya kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika zinapaswa kutatoa elimu ya jinsi ya kutambua ugonjwa huo na mbinu za kukabiliana nao.
 Vilevile wakuu wote wa Mikoa, Wadau wote wa mbegu, wakulima na wananchi kwa ujumla katika mikoa inayolima mahindi kwa kutegemea umwagiliaji au kilimo cha msimu cha kutegema mvua wanapaswa kutoa taarifa mapema endapo dalili zisizo za kawaida zitaonekana katika mashamba ya mahindi.
 Muya aliwashauri wakulima wote kuhakikisha kuwa wananunua mbegu zilizothibitishwa ubora na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (Tanzania Official Seed Certification Institute – TOSCI).
Sambamba na agizo hilo, wauzaji na wasambazaji wa mbegu nchini wanaagizwa kuzingatia Sheria ya Mbegu ya Mwaka 2003, kinyume chake watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 Muya alitoa wito kwa wananchi wote waliopo mipaka kutokuhamisha au kubeba mahindi kiholela kutoka nchi jirani bila kufuata taratibu za kisheria.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top