KOCHA mpya
wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp anataka kumsajili Nicolas Anelka Januari
mwakani.
Redknapp
atapewa pauni Milioni 10 za kusajili katika dirisha dogo, lakini atahitaji fedha
zaidi ili kuingia sokoni.
Nicolas
Anelka
Kocha huyo
mwenye umri wa miaka 65 anafahamu anatakiwa kuboresha safu yake ya ushambuliaji
kutokana na kukabiliwa na majeruhi Andrew Johnson na Bobby Zamora, wanaomfanya
abaki na Djibril Cisse kama mshambuliaji pekee.
Na Redknapp
amemtambulisha mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea, Anelka kama mtu
anayemtaka kwa mkopo.
Mkongwe huyo
mwenye umri wa miaka 33 ana mkataba na Shanghai Shenua, lakini anaweza kurejea
kuwa muda kucheza England, baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya
China.
Anelka kwa
ujumla yuko tayari kurejea Ulaya baada ya kusema alifanya kosa kuhamia
China.
Post a Comment