Katika soka la wanawake wenyeji wa michuano ya kuwania
kombe la frika kwa akina dada,timu ya taifa ya Equatorial Guinea wamefanikiwa
kunyakua kombe la mataifa ya AFRIKA baada ya kuichapa BANYANA BANYANA ya AFRIKA
KUSINI kwa magoli Manne kwa bila katika mchezo wa fainali ulichezwa
jana.
Magoli ya
Equatorial Guinea yamefungwa na Gloria Chinasa aliyepachika mawili, na mabao
mengine mawili yakafungwa na Tiga na Geneveva Ayonman.
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa mjini
MALABO wenyeji EQUATORIA GUINEA wametetea taji la AFRIKA kwa mara ya pili
mfululizo.
Kwa upande wao BANYANA BANYANA wameshindwa
kutimiza ndoto zao za kunyakua kombe la kwanza la mataifa ya AFRIKA
Post a Comment