Hayatou kushoto akiwa na Rais wa FIFA, Sepp Blatter kulia |
RAIS
wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou amekubali kuhudhuria sherehe za
ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
Cecafa-Tusker Challenge wiki ijayo mjini Kampala, Uganda.
Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rogers Mulindwa amesema leo kutoka Uganda
kwamba, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) tayari
limepokea uthibitisho wa Hayatou kufungua michuano hiyo kutoka makao makuu ya
CAF, Cairo, Misri.
Bosi huyo wa soka
barani, anatarajiwa kuwasili Kampala Novemba 22, kufuatia mwaliko huo wa Rais wa
CECAFA, Leodegar Tenga.
Rais wa FUFA, Lawrence
Mulindwa amesema Uganda imefurahia heshima hiyo ya ujio wa Hayatou, ambaye
atafuatana na viongozi mbalimbali wa CAF, akiwemo Katibu Mkuu, Hicham El Amrani,
Mohamed Raouraoua,
Constant Omari na
Ngangue Appolinaire. Katika ziara yake hito, Hayatou atahudhuria Mkutano wa
CECAFA katiuka hoteli ya Serena Ijumaa ya Novemba 23 kabla ya kufungua rasmi
michuano ya mwaka huu ya Cecafa-Tusker Cup Uwanja wa Namboole jioni ya siku
inayofuata.
Post a Comment