Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JESHI LA POLISI LAFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA


Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na.(022)2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.

 
02 Septemba 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP Said Mwema, amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani SACP Ernest Mangu anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kuziba pengo la marehemu ACP Liberatus Barlow, ACP David Misime aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya SACP Zelothe Steven anayestaafu. Vilevile, aliyekuwa kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.

Aidha, wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi na Makao Makuu Idara ya Upelelezi ambapo ACP Engelbert Kiondo kutoka makao makuu Idara ya Upelelezi anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi Kwenda kuwa Kamanda wa kikosi cha Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, ACP Shaban Hiki kutoka Kamanda wa Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas Mkondya kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha Ufundi.

Mabadiliko hayo pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa kikosi cha Usalama Barabarani ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia Mradi wa SMARTER Traffic ambapo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa RTO mkoa wa Pwani ACP Swalehe Mbaga. Uhamisho huo pia umewahusisha baadhi ya Wakuu wa Operesheni wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya.

Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:
Advera Senso-ASP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top