Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KATIBU MKUU WA BAKWATA ATOA USHAHIDI KESI YA AKINA PONDA

 

Mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo, Shehe Ponda Issa Ponda (kulia) na wenzake.
Ponda akirudishwa rumande.
Akiongoza kuelekea mlango wa mahabusu ya mahakama hiyo.
Waislam wakipiga takbirrr… wakati gari lililombeba Ponda na wenzake likiwapeleka Gereza la Segerea.
Askari wa kutuliza ghasia wakilinda usalama eneo hilo.
Gari lenye maji ya kuwasha nalo lilikuwa tayari kwa lolote.
Waislamu wakiondoka mahakamani hapo huku wakiilani BAKWATA kwa kuimba; “Bakwata laanakum… Bakwata laanakum… Bakwata laanakum”.
KATIBU Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini (BAKWATA), Suleiman Said Lolila, leo amepanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi jinsi Baraza hilo lilivyoipatia eneo la Chang’ombe Markas Kampuni ya Agritanza Ltd ambalo hivi karibuni w Waislamu walilivamia na kusababisha kesi inayounguruma mahakamani hapo. Ustaadhi Lolila alisema awali eneo hilo lilipangwa kijengwe chuo kikuu cha Kiislamu lakini lilianza kumegwa kidogokidogo na kubakia hekari nne hivyo ikabidi BAKWATA kupitia vyombo vyake ambavyo ni Mkutano Mkuu, Baraza la Ulamaa na Baraza la Udhamini kuona halitoshi kujenga chuo kikuu hivyo wakaafikiana kumtafuta mtu mwenye eneo kubwa wabadilishane naye. Baada ya kumtafuta mtu wa kubadilishana naye, wakaipata kampuni ya Agritanza ambayo iliwapa hekari 40 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho ambapo nao waliichachia kampuni hiyo hekari zilizopo Chang’ombe Markas kiwanja namba 311/3/4/Block/D/Chang’ombe.
Kesi hiyo iliendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Tumaini Kweka, ambapo upande wa utetezi alikuwepo Wakili Juma Nassoro. Mshitakiwa wa kwanza, Shehe Ponda Issa ameendelea kukosa dhamana.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top