Kwa mujibu wa Tume ya
Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, imetaja aina mbalimbali za dawa za kulevya
zikiwemo heroine, cocaine, bangi na mirungi.
Hata hivyo, dawa za kulevya zenye madhara makubwa kwa watumiaji ni ‘HEROINE’ ambayo ni aina ya dawa ya kulevya itokanayo na mmea unaojulikana kama Opium Poppy.
Dawa hiyo kwa mujibu wa Tume, hupumbaza mfumo wa fahamu na zinaingizwa nchini ikitokea nchi za Mashariki ya mbali kama Afghanistan, Pakistan, Thailand, Laos, India, Myanmar na nchi nyingine za Mashariki ya mbali.
“Dawa hii ina majina mengi mitaani, wengine wanaita ‘unga’, brownsugar, ngoma, ubuyu, mondo, poda, dume ama farasi,” inabainisha moja ya kijarida cha tume hiyo.
Hata hivyo, kijarida kinachozungumzia dawa aina ya heroine ni kwamba hutumika kwa kuvuta, kunusa unga, kunusa moshi ‘kuchesi’ na kujidunga ili kuongeza wingi wa dawa wauzaji wengi huongeza sukari, kahawa, asprini na panadol.
Mchanganyiko huu unakuwa ni hatari na sumu zaidi kwa watumiaji kinabainisha kijarida hicho.
Hata hivyo, watumiaji wengi wanakumbana na madhara ya dawa hiyo ambapo hujenga hali ya uteja kwa haraka sana kuliko dawa yoyote nyingine.
Utafiti unaonesha kuwa katika kila watu wawili waliojaribu kutumia heroine, mmoja wapo alifikia hali ya uteja, mtumiaji hupata usugu hali inayosababisha aongeze kiwango anachotumia siku hadi siku.
Madhara mengine ni kuwa mchafu na kuishi kwenye mazingira machafu, kukosa umakini, kuzubaa na kupunguza uwezo wa kufanya kazi, kuharibika kwa mfumo wa ubongo na fahamu.
Pamoja na hayo, imebainisha kuwa mtumiaji wa dawa hiyo anakumbwa na madhara mengine ya kupatwa na magonjwa ya moyo, ini kifua na mapafu.
Kadhalika, hupatwa na kigugumizi, kichefuchefu, kutapika na kufunga choo na kwa wanawake kujitokeza kwa mabadiliko ya hedhi, kushuka kwa mapigo ya moyo.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa dozi kubwa husababisha kifo na mchanganyiko wa heroine na pombe huleta madhara makubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kifo cha ghafla.
Watumiaji wa heroin kwa njia ya kujidunga husababisha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine ya damu kutokana na kushirikiana sindano na vifaa vingine.
Pamoja na madhara hayo, Kijarida hicho kimezungumzia madhara kwa watumiaji wenye ujauzito ni pamoja na kupata matatizo ya upungufu wa damu, moyo, mimba kuharibika, kuzaliwa watoto njiti.
Madhara mengine ni watoto kupata matatizo ya kiafya ikiwemo kuchelewa kukua kiakili na kimwili sambamba na kujifungua watoto ambao mara nyingi hufa wakiwa na umri chini ya miaka mitano.
Dawa nyingine zenye kuleta athari ni MIRUNGI, aina ya mimea inayostawi kwenye hali ya unyevunyevu na milima yenye urefu kati ya futi 4,000 hadi 9,000.
Hapa nchini mimea hiyo hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga, hata hivyo kiasi kikubwa cha mirungi itumikayo nchini hutoka Kenya.
Dawa hii kwa majina ya mitaani huitwa miraa, mbaga, mogoka, veve, gomba na kashamba, ambapo madhara ya mirungi ni kutokea matatizo ya kisaikolojia kama kukosa hamu ya kula, vidonda vya tumbo, mdomoni na kukosa choo.
Kwa mujibu wa kijarida hicho , madhara mengine ni kupungua maji mwilini, shinikizo la damu, kukosa hamu ya kufanya mapenzi, mwili kuwasha, maumivu makali ya kichwa kuharibika kwa ini na kupungua kwa nguvu za kiume.
“Mirungi husababisha mtumiaji kukosa usingizi kwa muda mrefu, hivyo kuongeza uwezekano wa kupata ajali wanafunzi kushindwa kuelewa masomo na mengine,” kinaelezea Kijarida hicho.
BANGI pia ni miongoni wa dawa za kulevya ambapo athari zake kwa watumiaji ni nyingi, ikiwemo ya kuumwa koo, kupata kikohozi na saratani ya mapafu.
Hata hivyo, bangi ni mmea wenye rangi ya kijani ambayo hutoa majani, maua na mbegu hutumika kama kilevi na bangi hustawi karibu na maeneo yote hapa nchini ambayo hutumika zaidi kuliko dawa nyingine za kulevya.
Bangi hupatikana kwa wingi katika Mikoa ya Mara, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Tabora, Tanga, Kagera na Mbeya.
Kwa upande wa majina ya mitaani imepewa majina mengi kama msuba, ganja, daga, jani, stiki, ndumu, kaya na msokoto ambapo wavutaji wa bangi hubakiza moshi mwingi kwenye mapafu kwa muda mrefu.
Hivyo moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji wa kazi wa mapafu.
Bangi ina kemikali sumu inayosababisha saratani zaidi ya tumbaku hivyo madhara yake kwa watumiaji ni makubwa zaidi.
Kutokana na uvutaji wa bangi, madhara yake ni makubwa, inaathiri mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi.
Pia kupungua kwa kinga ya mwili, kupoteza kumbukumbu, utegemezi sugukuchanganyikiwa, ukatili, ukorofi na uhalifu pamoja na mtumiaji kuridhika na hali duni aliyonayo, hivyo kukosa mwamko wa maendeleo huku akijihisi ni mwenye mafanikio makubwa.
Hivyo kutokana na madhara hayo ya matumizi ya dawa za kulevya, kila mmoja wetu analojukumu la kuhakikisha jamii haitawaliwi na matumizi ya dawa za kulevya.
Kwa mantiki hiyo, wazazi wanalo jukumu kubwa la kuwalea watoto ipasavyo kwa kujenga mawasiliano ya karibu, kuwasaidia kwenye matatizo yao na kuwafundisha kuhusu athari za dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Kijarida cha tume, kuwa tunapinga vita matumizi ya dawa za kulevya kutokana na ukweli kuwa jamii inayotawaliwa na dawa za kulevya hukosa amani na uhakika wa maisha kutokana na madhara hayo,yakiwemo kama ugomvi, uporaji, vita, uvunjaji wa sheria na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Post a Comment