Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MISS EAST AFRICA KUPATIKANA 07 DISEMBA, MLIMANI CITY



 
Mrembo atakayeiwakilisha Somalia katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu ametangazwa rasmi Mrembo huyo mwenye urefu wa futi 5.9 anaitwa HALIFA AYAN YUSUF aliyezaliwa Somalia Hargeisa na ana umri wa miaka 21.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltdya jijini Dar es salaam
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top