NEW YORK,
Marekani
MSANII
kutoka jijini New York, Keri Hilson, anayetamba na nyimbo zake kali kama ‘That
way you love me’, ‘Pretty girl Rock’ na ngoma nyingine, anatarajia kutua nchini
hivi karibuni kwa ajili ya kudondosha bonge la Shoo, ambapo pia atamalizia shaoo
yake nchini Kenya, Imeelezwa.
Taarifa
hizo zimetolewa na Msanii huyo katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa
Twitter, ambapo ameweka wazi kuwa anatarajia kuwasili nchini mwezi ujao wa
Desemba, ambapo amesema kuwa hiyo itakuwa ni mara yake ya kwanza kufanya Shoo
katika Nchi za Afrika Mashariki hususan kwa nchi kama Tanzania na
Kenya.



Post a Comment