Shirikisho
la soka Tanzania (TFF) limewataka Watanzania kutoibeza timu hiyo, badala yake
kuiunga mkono.
Stars ipo
nchini humo ikishiriki michuano ya Chalenji inayoendelea nchini humo, juzi
ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudan.
Rais wa
TFF, Leodger Tenga alisema jana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiibeza timu
hiyo na hasa kudai wachezaji wake wamezeeka kitu ambacho si cha kweli kwani
wengi wao wana miaka 28 kushuka chini.
Alisema
ni vizuri kuwatia moyo wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na ari kubwa,
hivyo kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo mikubwa.
Akizungumzia
mchezo wa leo, kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen alisema kwamba vijana wake wapo
kamili kwa mchezo huo na ili waweze kuifunga Burundi ni lazima wacheze kwa kasi
na pasi za haraka.
“Lazima
tucheze kwa kasi kubwa sana tena kushinda ule mchezo na Sudan Jumapili kwani
Burundi ni timu nzuri lakini tutawabana.”
Post a Comment