Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo tarehe 19 Nov.2012 |
Pili ,Katibu wa NEC alizungumzia pia ziara ya siku nne katika maeneo mbalimbali ikiwa moja ya harakati za kusukuma ilani ya uchaguzi ya CCM, Katibu mkuu ,Abdulrahamu Kinana ataongozana na viongozi wengine wa Sekretarieti pamoja na Mawaziri husika katika maeneo hayo.
Ziara hiyo itakayoanza tarehe 21 mkoani Mtwara ambapo masuala mbalimbali yanayohusu wakulima wa Korosho, Bandari na miundo mbinu mingine itafanyiwa kazi, tarehe 22 Katibu atakuwepo mkoa wa Rukwa ,Sumbawanga kuangalia maendeleo ya miradi barabara, tarehe 23 Geita, Migodi na masuala ya wachimbaji wadogowadogo,na kumalizia Arusha tarehe 24,ambapo kuna viwanda vingi ambavyo vipo chini ya wawekezaji lakini havifanyi kazi, na kusababisha tatizo la ajira na uchumi kudorora.
Post a Comment