
Shughuli za uokozi
zilivyoendelea
Juhudi za uokozi katika
jengo la ghorofa lililoporomoka wiki jana nchini Ghana
zimesitishwa.
Kwa mujibu wa maafisa
waliokuwa wanasimamia shughuli hiyo, mjini Accra, idadi ya watu waliofariki
imefika 14, wala sio kumi na nane kama ilivyoripotiwa hapo awali huku watu
wnegine 67 wakinusurika.
Mmiliki wa jengo hilo, pamoja na afisaa anayesimamia ubora wa majengo, wamezuiliwa.Ujenzi mbovu umelaumiwa kwa kuanguka kwa jengo hilo lenye maduka na amblo lilifungua rasmi mapema mwaka huu.
Rais John Dramani
Mahama, alisema kuwa wale waliohusika na kupuuza usalama na ubora wa jengo hilo
lazima watachukuliwa hatua kali.
'manusura wangali
hospitalini'
Msemaji wa jeshi,
kanali, M'bawine Atintande alisema siku ya Jumapili kuwa waokoaji waliweza
kufika eneo la chini ya jumba hilo na kwamba hawakuwa na matumaini ya kupata
manusura zaidi.
Takriban watu 81
waliokolewa kutoka chini ya vifusi, kumi na wanne kati yao wakiwa wamefariki
alisema kanali bila ya kuelezea kwa nini waokoaji walikuwa wamekadiria wale
waliofariki kuwa 18.
Kati ya manusura 67
waliopelekwa hospitalini, 13 wangali wanapokea matibabu huku 54 wakiruhusiwa
kwenda nyumbani.
Afisaa mmoja alihojiwa
na kisha kuachiliwa kwa dhamana.
Mnamo siku ya Alhamisi,
idara ya uhandisi nchini humo, ilisema kuwa jengo hilo halikuwa na kibali
kumaanisha kuwa huenda halikukaguliwa kabla ya kufunguliwa rasmi


Post a Comment