Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) imeanzisha utaratibu wa kuwasilisha taarifa za marejesho ya kodi
kwa njia ya mtandao kwa lengo la kuboresha na kurahisisha uwasilishaji wa
taarifa hizo.Kaimu Mkurugenzi wa TRA, Allan Kiula, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa lengo la kuanzisha utaratibu huo ni kuwapa fursa walipakodi kuhifadhi taarifa zao katika kopyuta kwa ajili ya kumbukumbu zao na kurahisisha uhakiki wa taarifa zinazotumwa.
Alisema lengo lingine ni kupunguza uwapo wa makosa kwenye taarifa zinazotumwa na kuondoa msongamano kwenye ofisi za mamlaka ya mapato.
Kiula alisema kupitia utaratibu huo, walipa kodi watawasilisha taarifa za marejesho ya kodi zao wakiwa mahali popote pale, hususan majumbani au ofisini.
Alisema watakaokuwa wanatuma taarifa kwa njia ya mtanadao, ni wale, ambao watakuwa wamejisajili pekee na dole gumba.
Aliwataka ambao hawajajisajili, kujisajili ili waweze kutumia utaratibu huo.
habari NA ELIZABETH
ZAYA
CHANZO:
NIPASHE


Post a Comment