Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na
ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Tanzania waliofika ofisini
kwake Migombani. Katikati ni kiongozi wa ujumbe huo Brigedia Jenerali JM
Mwaseba.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea zawadi kutoka kwa
kiongozi wa ujumbe wa wananchi wa chuo cha ulinzi cha Taifa huo Brigedia
Jenerali JM Mwaseba
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim
Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha ulinzi
cha Taifa Tanzania waliofika ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.Picha na
Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar
----
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema suala la amani na
usalama ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu
wake.
Amesema
suala hilo linapaswa kuzingatiwa na kufanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa amani ya
Tanzania inaendelea kuwepo wakati wote kwa lengo la kuendeleza sifa ya Tanzania
kiusalama, sambamba na kukuza uchumi wa nchi.
Maalim Seif
ametoa changamoto hiyo leo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokuwa na
mazungumzo na ujumbe wa wanafunzi wa chuo cha ulinzi cha Taifa Tanzania
(National Defence Collage) cha Dar es Salaam, waliofika ofisini kwake kwa ajili
ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo.
“kulinda
amani ya nchi yetu ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya taifa ya taifa letu, na
nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuanzisha chuo hichi”,alieleza.
Amesema
nchi zilizoendelea na zina zinazoendelea kwa kasi zilianza kazi ya kulinda
usalama wa nchi zao kwa kipindi kirefu, na ndio maana ziliweza kupata mafanikio
katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii. Amesema ni vyema vyombo vya
ulinzi na usalama kuanza kudhibiti viasharia vya uvunjifu wa amani mara
vinapogungudua hali hiyo, ili kuiepusha nchi kuingia katika janga la uvunjifu wa
amani.
Aidha
amesema katika kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani serikali inapaswa
kujipanga kukabiliana na kero za wananchi hasa ukosefu wa ajira kwa
vijana.
Makamu wa
Kwanza wa Rais amefahamisha kuwa vijana wengi ambao wamehitimu masomo katika
fani mbali mbali bado hawana ajira na kwamba hali hiyo inaweza ikawapelekea
vijana hao kufanya vitendo visivyokubalika katika
jamii.
Kwa upande
wake kiongozi wa ujumbe huo Brigedia Jenerali JM Mwaseba ameelezea matumaini
yake kuwa wahitimu wa chuo hicho wataweza kuongeza ujuzi wao katika masuala ya
ulinzi na usalama na kusaidia mabambano dhidi ya vitisho na vitendo vya uvunjifu
wa amani.
Amefahamisha kuwa wahitimu wa chuo hicho pia watakuwa
ni watunga sera wazuri katika taasisi wanazotoka, lengo likiwa ni kuimarisha
hali ya usalama na kuimarisha uchumi wa nchi.
Jenerali
Mwaseba ameongeza kuwa kozi hiyo ya mwaka mmoja kwa kuanzia imewashirikisha
wanafunzi wa Tanzania pekee kutoka taasisi mbali mbali za serikali Muungano na
Zanzibar wakiwemo watendaji kutoka Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi na Taasisi
za kiraia.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Zanzibar


Post a Comment