Staa kutoka ’game’ ya muziki wa kizazi kipya Bongo,
Herry Samir ‘Mr Blu’ amesema nguvu ya zaidi ya 10 aliyoiweka kwenye fani hiyo
sasa imemfanya kumiliki kiasi kikubwa cha ‘ngawira’ za kibongo
(Shilingi).
Katika Interview ya dakika 45 aliyoifanya na moja ya
mtandao maarufu nchini, juzi kati, Blu ambaye sasa yuko kwenye kilele cha Bongo
Fleva akisumbua na ngoma yake mpya inayobeba jina la ‘Nipende kama nilivyo’
alifunguka kuwa si mara moja mtu anaweza kuzungumza juu ya kile kinachomhusu
kama anachokifanya yeye lakini ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuwaonyesha
watu kuwa kile wanachokifanya wasanii ni kazi ama bishara kama zilivyo
zingine.
“Kwanza, nashukuru kwa kuwa umenifuata na kuniuliza
mambo kama hayo, ukweli ni kuwa nafahamu ni ngumu kwa mtu kuzungumza juu ya
vitu kama hivyo lakini kwa kuwa tunachokifanya wasanii ni kazi kama zilivyo
zingine sina tatizo nitakujibu kila kitu katika ukweli na kwa ufupi sana”
alisema Blu.
Akiendelea Blu ambaye pia mashabiki wake hupenda
kumuita ‘Babylon Baysser’ alisema kufanikiwa kwa wimbo wake wa kwanza ‘Niite
Mr Blu’ ndiyo ulikuwa mwanzo wa mafanikio licha ya matatizo kadhaa aliyokutana
nayo mara baada ya kupata umaarufu.
“Kulikuwana matatizo mengi sana baada ya kufanikiwa
kwa ngoma hiyo, lakini nashukuru Mungu kuwa ndani ya muda wote huo nimefanikiwa
kujenga nyumba yangu,kununua gari, na pia akaunti yangu kwa sasa iko poa
sana”,
“eee ndiyo natarajia kuoa, na kwa kuwa
tayari nina mtoto haina shaka kuwa mama mtoto wangu ndiye nitakayempa heshima
hiyo” kwa hiyo hicho ndiyo ninachoweza kusema kuwa huo ndiyo utajiri wangu
ndani ya miaka zaidi ya 10 kwenye gemu kwa kuwa nimetumia nguvu zangu kupata
vitu hivyo vyote na siku zote Mungu amekuwa akinisimamia” alisema mr blue
Post a Comment