Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Walimu wapya 28,638 sasa kupelekwa vijijini

Serikali imetangaza mpango mpya wa ajira za walimu 28,638 wa Shule wa Msingi na Sekondari katika mikoa minane.

Mikoa hiyo ni ile ambayo inakabiliwa na changamoto ya uduni wa miundo mbinu, mazingira bora ya kufanyia kazi na kukosa motisha kwa wafanyakazi kama vile nyumba za kuishi.

Utaratibu huo wa ajira mpya hautahusisha majiji na manispaa ambako walimu wengi hukimbilia baada ya kupata ajira na serikali imepanga kuwachukulia hatua watumishi wake zaidi 800 waliotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu bila idhini ya mwajiri.

Hatua hiyo ilitangazwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzi, Philipo Mulugo, aliyoitoa wakati akizungumza na wahitimu zaidi ya 700 wa Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo mkoani Iringa.

Mulugo alisema licha ya kuamua kuajiri walimu 28,638 idadi ya walimu wote waliohitimu kwenye vyuo vinavyotoa mafunzo hayo havikamilishi idadi hiyo.

“Wote hapa, tutawaajiri, lakini safari hii, hakuna ajira mijini na wote mtakaoajiriwa, tunawapeleka katika wilaya zenye changamoto, kwa hiyo mtakwenda mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Shinyanga, Manyara, Mtwara na Lindi. Tamko la serikali ndio hilo na mfahamu kabisa kwamba ajira hizi hazitahusu majiji na manispaa,” alisema Mulugo.

Alisema ajira hizo zitangazwa rasmi Januari mwaka 2013 huku akionya kuwa wahitimu hao wa shahada ya kwanza ya ualimu katika fani mbalimbali wasithubutu kuwashawishi maofisa waandamizi wa wizara kuomba kuteuliwa kuwa maofisa elimu wa wilaya na mikoa.

Kuhusu walimu waliotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pasipo ridhaa ya mwajiri, Mulugo alisema serikali imegundua kuwa tatizo hilo limeiathiri zaidi mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa na na mikoa ya Kaskazini ambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu.

“Nawatangazia kiama wale ambao walitoroka kazini na kuja kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pasipo ridhaa ya mwajiri wake…Wizara imewaagiza maofisa elimu wa Wilaya na Mikoa kuleta haraka majina hayo wizarani ili tuchukue hatua kali,” alisema Mulugo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Prof. Amandina Lihamba, akizungumzia changamoto zinazoikabili MUCE, alisema baadhi ya miradi ya ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu chuoni hapo kwa sasa imekwama na hivyo kuathiri shughuli za taaluma.

“Tumepokea kutoka Hazina kiasi cha Silingi bilioni 1.3 zilizoidhinishwa na serikali, lakini baadhi ya miradi tunayoiendesha imekwama na kuathiri shughuli za taaluma kwa ujumla,” alisema.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala, alisema kuwa MUCE kimekumbana na changamoto za uongozi na utawala na kwamba bodi ya chuo hicho imelazimika kufanya mabadiliko katika ngazi mbalimbali za utendaji.


CHANZO: NIPASHE

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top