Wenza wa
viongozi yaani mke au mume, viongozi wa dini na watoto wenye umri chini ya miaka
18 wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea uvunjaji wa maadili
nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda alipokuwa akizungumza wakati wa
hafla ya Uzinduzi wa Tovuti ya Sekretarieti
hiyo.
Kamishna
huyo alisema wenza wa viongozi wanayo nafasi kubwa ya kukemea uvunjaji wa
maadili pale anapomuona mwenzake anafanya hivyo ili kuhakikisha wanafuata
maadili yanayostahili.
Kamishna
huyo pia amewaomba viongozi wa dini nao wasaidie kukemea vitendo vya ukosefu wa
maadili kwa waumini wao. Aliongeza kuwa kama kuna desturi ya kuungama dhambi
basi viongozi wa dini wawakumbushe waumini wao kufanya
hivyo.
Akizungumzia
watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao sheria ya Maadili pia inawagusa,
Kamishna Kaganda alisema wanayo nafasi kubwa ya kuwakumbusha kwa heshima na bila
kuwakosea adabu wazazi wao wajibu wao na kuwaeleza wazi kwamba Cheo ni dhamana
wasikichezee ili kuwalinda.
Alisema
suala la ukosefu wa maadili katika makundi mbalimbali ya jamii limekuwa ni janga
la kitaifa hivyo aliwataka watanzania kurudi kwenye Utamaduni wa
Kitanzania.
Kamishna
Kaganda alisema fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni pia zitapatikana kwenye
tovuti iliyozinduliwa leo na kwamba hivi sasa zimeshasambazwa kwa viongozi wote
wa Umma, na wanatakiwa kuzijaza na kurejesha kabla au ifikapo Disemba 31 mwaka
huu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Alisema
kiongozi yeyote atakayekiuka Agizo hilo la serikali atachukuliwa hatua kwa
mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995. Aliongeza
kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo kifungu (i), kiongozi anapaswa kujaza fomu hizo
katika siku 30 baada ya kupewa wadhifa wake, kila mwisho wa mwaka wa kalenda na
mwisho wa kutumikia wadhifa au cheo chake.
Akizindua
Tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu- Ikulu Bibi Susan Mlawi alisema Tovuti hii ni
muhimu kwa kuwa itarahisisha upatikanaji wa huduma na habari mbalimbali kwa
lengo la kuelimisha Umma pamoja na kuwajengea wananchi uwezo wa kupata taarifa
muhimu kupitia teknolojia ya Habari na mawasiliano yaani
TEHAMA.
Alisema
Tovuti aliyoizindua pia itawawezesha viongozi wa Umma nchini kote kupata na
kujaza Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni na hivyo kuziwasilisha Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa
wakati.

Post a Comment