Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM YAIGARAGAZA VIBAYA CHADEMA KWENYE UCHAGUZI MDOGO


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani Kyela, vimechuana vikali kwenye uchaguzi mdogo wa vijiji na vitongoji uliofanywa kuziba nafasi mbalimbali zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Nafasi zilizokuwa zikiwaniwa ni wenyeviti wa vijiji 13 na vitongoji 61 ambapo vyama vya CCM, CHADEMA na TLP vilijitokeza kuwania nafasi hizo ingawa TLP hawajaambulia nafasi yoyote.

Taarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi huo wilaya ya Kyela, Omary Mungi, ilieleza kuwa CCM ilishinda katika vijiji nane na CHADEMA imeshinda katika vijiji vitano na katika nafasi ya vitongoji, CCM wamepata vitongoji 50 na CHADEMA 11.

Chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top