Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA INAUMALIZA MWAKA VIBAYA KWA MWENDELEZO WA MAKAMANDA WAKE KUCHANA MAGWANDA

KUJIVUA UANACHAMA WA CHADEMA KUACHIA NYADHIFA ZOTE ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA NA KUJIVUA UANACHAMA WA CHADEMA


Ndugu wanahabari naomba mnifikishie taarifa hii kwa Watanzania
wenzangu wenye uchungu na nchi hii;
Deogratius Kisandu (kulia)
1.1. UTANGULIZI
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na hisia hasi juu yangu na mkoa wa Tanga
kwa ujumla juu ya ushiriki wangu kwenye shughuli za chama. Natambua
kwamba wapo ambao tayari wameniona mnafiki, mamluki na msaliti
kwasababu tu ya kutopenda kutambua ukweli juu ya mwenendo wa chama
changu cha CHADEMA.
Nimeamua kuandika waraka huu nikitambua ya kwamba, kutambua ukweli ni
njia ya kuibua fikra chanya, kuamini matendo chanya kuelekea kupata
mafanikio zaidi. Ni heri kuzungumza ukweli ulio wazi kuliko kuwa
kondoo na mnafiki ndani ya chama. Kupitia barua hii naomba nitoe
dukuduku langu la moyoni kwa manufaa ya chama changu cha CHADEMA.
1.2.UCHAGUZI WA 2010.
Mwaka wa 2010 nilikuwa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Sebastian
Kolowa(SEKUCo). Kwa ujasiri mkubwa niliamua kuchukua fomu na kugombea
ubunge kupitia CHADEMA jimbo la Lushoto mkoani Tanga, japo kuwa sikuwa
mzawa wala mkazi wa Lushoto.
Pamoja na kujenga mazingira mazuri kisiasa, nasikitika kusema kwamba
viongozi wa chama changu ngazi ya Taifa wamekuwa wepesi sana kupuuza
mkoa wa Tanga ikiwamo wilaya ya Lushoto katika ujenzi wa chama.
Wamekuwa wepesi sana kulaumu viongozi wa chama kuliko kufika katika
maeneo husika na kuona hali halisi. Kumbukeni kwamba tangu uchaguzi
wa 2010 mkoa wa Tanga umesahaulika kabisa na kususia viongozi wa
wilaya na majimbo. Vilevile ikumbukwe kwamba ujenzi wa chama ni kazi
ya kujitolea, hivyo kazi hii haiwezi kufanikiwa bila mawasiliano
mazuri na viongozi wa kitaifa.
1.2. CHAGUZI NDOGO ZA MADIWANI.
Uaminifu finyu kwa viongozi wa chini wa chama ni sababu ya kufanya
vibaya. Kumekuwepo na mgawanyo mbovu wa madaraka ndani ya chama
unaokiuka misingi ya katiba ya chama. Kumejengeka utamaduni wa
viongozi wa juu wa chama kuhodhi madaraka ya viongozi wa chini wa
chama na kuvuruga utendaji wa viongozi kwa kisingizio kwamba viongozi
wa chini ni mamluki takribani nchi nzima. Hatuwezi kupata mafanikio
makubwa ya kisiasa na kujenga mtandao imara wa chama kama tutaendelea
na utamaduni huu wa kudharau viongozi wa chini wa chama.
1.3. ZIARA ZA M4C.
Ziara za M4C zimekuwa za kiupendeleo zaidi bila kuzingatia maeneo
ambayo hayakufikiwa na kampeni za Urais mwaka 2010. Mkoa wa Tanga
umekuwa ukitengwa sana na kutokuthaminiwa katika ujenzi wa chama.
Pamoja na ukweli kwamba chama kimejengwa kwa misingi ya kujitolea,
ubinafsi wa viongozi ni kikwazo kikubwa kwa CHADEMA. Ushindi wa
CHADEMA hautatokana na baadhi ya mikoa ya Tanzania bali wastani mzuri
wa kura kwa kila mkoa wa Tanzania.
Ninashindwa kuelewa vigezo vya M4C katika kuchagua viongozi
wanaotakiwa kushiriki ziara za vuguvugu la mabadiliko(M4C).
Inanishangaza kuona mwanachama aliyejiunga jana CHADEMA akitokea CCM
leo anapewa kipaumbele kuliko viongozi waliojenga chama kwa muda mrefu
kwa nguvu ya kujitolea hasa ma wilayani, majimboni na mikoa kwani
viongozi hawa wa chini hawalipwi chochote zaidi ya nguvu zao na mwisho
wa siku wanaitwa majina mengi mara mamluki, wasaliti, wametumwa na
CCM. Kwa mwendo huu hatuwezi kufika wakati viongozi waliopo juu
wanalipwa mishahara na wanaojenga chama huku chini wanaitwa majina ya
kila aina.
1.4. UDHAIFU WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA(BAVICHA).
Baraza hili limeshindwa kabisa kufanya kazi yake ya kuwa unganisha
vijana bali limekuwa ndio chanzo cha migogoro. Migogoro yote
inayoendelea CHADEMA hivi sasa inatoka na Baraza hili kutokuwa makini
na utendaji kwani imekuwa kila mtu ni kibaraka, mamluki, kirusi,
anatumiwa hata kama anaongea ukweli, je tukipewa nchi nani atasimamia
rasilimali za nchi?
Unaweza sema baraza linafanya kazi kwa maana ya Mwenyekiti na Katibu
wake. Tunaposema baraza tunamaanisha wajumbe wote wa majimbo, wilaya
na mikoa wanashiriki vipi kujenga chama kupitia Baraza lao. Ukiangalia
vikao vya Taifa vya BAVICHA tangu vianze vimekuwa vikishirikisha
wenyeviti wa mikoa kinyume na katiba ya chama na mwongozo wa Mabaraza
upande wa BAVICHA ibara ya 6.8.6 wajumbe wa kamati tendaji ambapo
makatibu wa mikoa ni wajumbe lakini kinyume chake kikao kilichofanyika
Morogoro mwaka huu walishiriki wenyeviti badala ya makatibu tena
makatibu tumekuwa tukiletewa taarifa na wenyeviti. Lazima demokrasia
ichukue mkondo ndani ya chama tusifanye mambo kwa kupeana fadhila za
uchaguzi. Na hii ni ukritimba ndani ya chama na ulafi wa madaraka.
1.5. BUSARA IMEPOTEZA MWELEKEO CHAMANI.
Si kila mwenye kosa anastahili kuvuliwa uanachama, ukombozi wa
watanzania unahitaji kulindana na kujengana kwani wapinzani bado tuko
wachache sana, wengi ni mashabiki tu. Tunapofukuzana kwa makosa
madogomadogo hatujengi chama bali tunaongeza chuki na kupoteza imani
kwa wananchi. Mgogoro wa madiwani wa Arusha na Mwanza haikuwa njia
nzuri ya kuwafukuza madiwani bali ilitakiwa kuwajenga na kuwa fanya
wawe imara. Unajua hata mamluki kama wanavyo dai kwenye mitandao ya
kijamii wanaweza kubadilika kwa busara nzuri.
Nakumbuka hata kule nyumbani kwetu wilaya ya kahama viongozi waliokuwa
kamati tendaji ya jimbo la kahama pamoja na aliyekuwa mgombea wa
ubunge walivuliwa uanachama na Mwenyekiti wa wilaya na viongozi wa
Taifa wakabariki, nimesikia majuzi tu mwezi desemba 2012 kule Mbeya
kuna viongozi wamevuliwa uanachama. Hizi ni sampo tu.
Style hii ya vuavua uanachama haitawezesha chadema kushika dola, kwani
chama makini hakifukuzi bali humjenga mtu ili abadilike. Mimi binafsi
na kerwa sana na hali hii ya fukuzafukuza kwa kutumia kigezo cha
Katiba ya chama, watu wamekuwa wakikomoana kupitia katiba ya chama ili
kuoneshana ubabe. Hii hata mikoani imetawala sana kutokana na hofu ya
baadhi ya watu kutaka kuwa viongozi au baadhi ya viongozi kuonekana
wanang’aa kisiasa au kukubalika kuliko wengine. Hii pia kisaikolojia
inaweza kuwa ni hofu ya wabunge kuzidiwa kete na baaadhi ya vijana au
viongozi majimboni na wilayani na kuogopa kukosa nafasi zao kipindi
kijacho.
1.6. USHAURI WANGU.
Kama CHADEMA ina dhamira ya dhati ya kushika dola basi itambue mtu au
kiongozi anapo dai haki msimwite mamluki au katumwa na CCM hii
itasaidia kujenga chama, kwani viongozi wanajua fika mawazo yao katika
vikao hayawezi kukubalika kutokana na imani na kuabudu watu badala ya
kufata misingi ya chama.
1.7. URAIS 2015
Tangu nilipotangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
2015 viongozi wajuu wamekuwa wakijikanyagakanyaga na kuhoji nani
kamtuma huyu kijana. Chadema hakuna demokrasia ya kweli ndani ya chama
kwani watanzania mmeona wenyewe John Shibuda alipotangaza kuutaka
urais akaitwa mamluki, msaliti. Na Zitto Kabwe alipotangaza kuutaka
Urais anaitwa majina mengi mara msaliti, ooh anatumika na CCM. Sasa
mimi nashindwa kuelewa nini maana ya demokrasia, au nani anafaa kusema
anataka kuwa Rais ndani ya chama.
Nchii hii sasa ina siasa za kiliberali, tumeshatoka kwenye siasa za
Chama Kimoja ambao ulikuwa ni mfumo wa Chama cha Mapinduzi. Sasa kama
mambo yenyewe ndio hivi CCM itatuwia vigumu kuwapokonya utawala.
Nilichojifunza ndani ya chama wanaogopa kasi ya vijana wenye uwezo
walioko chini na kuanza kuhofu nafasi zao, ndio maana wengine wanasema
BAVICHA wanatakiwa waheshimu wakubwa(ARFI awaonya bavicha-Mtanzania ya
29/12/2012). Hivi hawa wakubwa waheshimiwe hata kama wanatupeleka
kusiko.
Urais ni uwezo wa mtu na karisma ya mtu, kama wewe huwezi muache
mwenzako, wewe unapiga kelele eti Kisandu hawezi kuwa Rais, sawa mbona
wewe hujatangaza nia ya kuwa Rais? Tuache ujinga wa kuendekeza kila
kitu kinacho semwa na Fulani ndio sahihi. CHADEMA kuna wanachama wa
aina tatu 1. walio anzisha chama 2. waliokipokea chama na 3. wanachama
waliowapatikana kipindi cha uchaguzi mkuu 2010 amabapo na mimi
nilikuwa mgombea wa ubunge jimbo la Lushoto na baada ya uchaguzi mkuu
huo, hawa wanachama namba3 hawa kijui chama vizuri wao wanaenda na
upepo tu, yaani kiongozi wa juu akisema kitu Fulani ni sahihi hata
kama kakosea au anataka ushauri. Ona Chadema tuko mstari wa mbele
kuipinga CCM na serikali yake kwa uongozi mbovu, sasa naomba vyama
vyote vya siasa hasa viongozi wa juu hapa Tanzania acheni ubinafsi na
ukritimba wapeni nafasi vijana msiwabanie.Jifunzeni kutoka Kenya
jirani zetu muone walivyo pewa vijana nafasi za kutetea nchi yao.
Mambo kama haya ndio yaliyo mfanya mwenyekiti wa vijana wa ANC Afrika
kusini kuvuliwa uanachama. Hebu turuhusu demokrasia.
1.8. HITIMISHO.
Nachukua maamuzi magumu japo mtaona nimekurupuka au nimepoteza dira
lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. Naachia nyazifa zote za uongozi
nilizo nazo ndani ya chama(Katibu wa BAvicha mkoa wa Tanga na Kaimu
katibu wa wilaya ya Lushoto) na ninajivua uanachama wa Chadema na
kubaki mwanachi huru.Fanyieni kazi niliyowaambia kuimarisha chama.
Maamuzi ya kujiunga na chama kingine ni demokrasia. Msimamo wangu wa
Urais uko palepale .
DEOGRATIUS KISANDU.
ALIYE KUWA KATIBU WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA(BAVICHA)
MKOA WA TANGA.
.29/12/2012
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top