Na Rajab Ramah, Nairobi
Mfululizo wa mashambulizi ya mabomu na
makombora ya hivi karibuni katika kitongoji cha Nairobi cha Eastleigh umefanya
wakazi wawe katika hofu na maafisa kuwa na wasiwasi juu ya matendo yanayoendelea
ya vurugu yanayokusudiwa kuchochea migongano ya kikabila na kidini nchini
Kenya.

Maafisa polisi wa
Kenya wakilinda eneo lilipotokea shabulio la makombora matatu tarehe 16 Disemba
lililolenga baa katika kitongoji cha Eastleigh mjini Nairobi. [Na Tony
Karumba/AFP]
Mashambulizi ya hivi karibuni yalianza mwezi
Novemba na kuendelea mwezi mzima uliopita. Hapo tarehe 18 Novemba, watu wanane
waliuliwa na dazeni kujeruhiwa katika mlipuko wa basi dogo uliotokea huko
Eastleigh. Shambulio hilo lilizuamapambano ya baina ya makabila kwa muda wa siku
mbili ambayo yalipelekea kujeruhiwa kwa watu 10 na kuharibiwa kwa mali
nyingi.
Hapo tarehe 5 Disemba, bomu la kutegwa kando ya
barabara liliua mtu mmoja na kuwajeruhi wanane wengine huko Eastleigh. Siku
mbili baadaye,guruneti lilivurumishwa katika kundi la waumini waliokua wakitoka
katika msikiti maarufu wa Hidaya. Mlipuko huo uliua watano na kujeruhi wengine
16, akiwemo mbunge na mlinzi wake.
Serikali ilianzisha msako wa usalama kufuatia
milipuko hiyo, na kuwatia mbaroni washukiwa 600, wengi wao wakiwa wahamiaji
haramu wanaoishi nje ya makambi ya wakimbizi ya Dadaab, kwa mujibu wa maafisa wa
eneo hilo.
Lakini milipuko imeendelea kuitikisa Eastleigh.
Siku ya tarehe 16 Disemba, watu wawili walijeruhiwa vibaya sana wakati kiasi
chamakombora matatu yalilengwa katika baa karibu na msikiti wa Hidaya. Polisi
waliwakamata washukiwa tisa kuhusiana na shambulio hilo.
Siku mbili baadaye, milipuko miwili iliwajeruhi
kiasi cha watu wawili karibu na msikiti kwenye eneo la Panganihuko Eastleigh.
Polisi aliwakamata watu 23 baada ya milipuko hiyo na kuwasaili ili kujua kama
wana habari zozote muhimu juu ya mashambulizi hayo, kwa mujibu wa Mkuu wa polisi
wa Nairobi Moses Nyakwama.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na mfululizo
wa mashambulizi haya, lakini maafisa kwa kiasi kikubwa wanawalaumu wanamgambo wa
al-Shabaab, wenye uhusiano na al-Qaida, ambao wameapa kutekeleza mashambulizi ya
kulipiza kisasi nchini Kenya ili kupinga uwepo wa Jeshi la Ulinzi la Kenya
nchini Somalia.
Serikali ya Kenya yaanzisha tume ya
uchunguzi
Ili kufikia kwenye kiini cha mashambulizi ya
karibuni ya kigaidi na kutafuta suluhisho, serikali itaunda tume ya uchunguzi ya
watu kumi, yenye maafisa wa serikali watano na wajumbe watano watakaopatikana
kutoka jamii ya wafanyabiashara wa Eastleigh.
Uamuzi wa kuundwa kwa tume hiyo ulikuja
Alhamisi (tarehe 20 Disemba) baada ya Waziri Mkuu Raila Odinga kuongoza mkutano
na Waziri wa Uhamiaji Otieno Kajwang, Waziri wa Maendeleo kwa Kaskazini ya Kenya
na Maeneo Mengine yenye Ardhi Kame Mohammed Elmi, Mkurugenzi Mkuu wa Kikosi cha
Intelijensia ya Usalama wa Taifa Michael Gichangi, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Usalama wa Ndani Mutea Iringo na wafanyabiashara wa Eastleigh.
Wajumbe wa tume hiyo bado hawajatajwa, lakini
polisi, Idara ya Intelijensia ya Usalama wa Taifa, Waziri wa Maendeleo ya
kaskazini mwa Kenya na Ardhi Nyingine Kame, Wizara ya Uhamiaji na ofisi ya
waziri mkuu, kila moja itachagua mjumbe moja. Kwa kuongezea, wawakilishi wa
wafanyabiashara watateuliwa na mwenyekiti wa Chama cha Wilaya ya Biashara
Eastleigh Hassan Guled.
Tume hiyo ambayo itaongozwa na Iringo, itapaswa
kuanza kazi mara moja, ofisi ya waziri mkuu ilisema katika taarifa kwa vyombo
vya habari.
Odinga alielezea wasiwasi wake kwamba
mashambulizi ya mara kwa mara ya kigaidi huko Eastleigh yanaharibu sura ya Kenya
na yanaangamiza sekta ya utalii. Aliipa kazi timu hiyo ya kutafuta sababu za
mashambulizi hayo na kutatua tatizo papo hapo ili kushughulikia hali hiyo.
Waziri mkuu aliwaomba wananchi kushirikiana na
tume ya uchunguzi kwa kutoa habari muhimu zitakazosaidia kuwasafisha magaidi na
wafuasi wao.
"Ninaitaka jumuiya ya wafanyabiashara katika
Eastleigh na wenyeji vilevile, kujitolea kwa kutoa habari yoyote ambayo
itawezesha kuwakamata wahalifu hawa na kuwapeleka mbele [ya sheria]," Odinga
alisema katika taarifa.
Alilaani kuinyooshea vidole kikabila jamii ya
Wasomali na kusema kuwa hiyo imepelekea mashambulizi ya kikabila dhidi ya watu
wasio na hatia na lazima hilo lisitishwe. "Kisilaumiwe kikundi chochote cha
kikabila kwa makosa yaliyofanywa na mtu mmoja miongoni mwao," Odinga
alisema.
"Kama sehemu ya suluhisho kwa mashambulizi haya
ya kigaidi, tunataka kuendesha elimu ya uraia katika maeneo yaliyoathiriwa ili
kuwahamasisha watu dhidi ya kujihusisha na shuguli za kigaidi au kuwaunga mkono
wahalifu," alisema wakati wa mkutano katika ofisi yake siku ya Alhamisi.
Jamii ya Eastleigh yajibu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wilaya ya Biashara
Hassan Guled aliiambia Sabahi kuwa anakaribisha hatua ya serikali kwa vile
ukuaji wa hali ya kutokuwepo kwa amani sio tu imechukua maisha ya watu, bali
imeharibu biashara pia.
Alisema kuwa mashambulizi ya maguruneti
yalikuwa yanaangamiza mahusiano baina ya Wakenya wenye asili ya Somalia na jamii
nyingine zinazoishi katika eneo hilo.
"Kile kinachokuwa kinaendelea hapa Eastleigh ni
aina fulani ya kupambana na moto [baina ya wahalifu na jamii] ambapo kila mtu
[kwa kutumia vurugu] baada ya shambuio la kombora ... lakini ni matumaini yetu
kuwa timu hii itasaidia [kufichua] nyuso zilizoko nyuma ya mashambulizi haya na
kuzuia matendo ya kihalifu yasitendeke kwa muda mrefu," alisema.
Guled aliwataka wananchi kushirikiana na timu
ya uchunguzi na kuwaomba polisi wasiwaachie huru washukiwa wa kigaidi ambao
wamekamatwa, kwa kusema kuwa tendo kama hilo litarudisha nyuma juhudi za
kudumisha usalama.
Wakati huo huo, wakazi wa Eastleigh walipokea
tangazo kuhusu tume mpya kwa hisia mchanganyiko.
Said Ali, mwenye umri wa miaka 30 na muuza duka
katika Garissa Lodge huko Eastleigh, alisema kuwa alikuwa na matumaini kuwa
mkabala huo mpya wa serikali utasaidia kuzuia mashambulizi, pamoja na kuzuia
polisi wasiitenge jamii ya Somalia.
"Ingawaje kumekuwepo [na jamii] iliyopigwa sana
na mashambulizi haya, serikali daima imekuwa ikijibu maeneo yaliyotokea milipuko
hapa kwa kutoa adhabu ya kuwahusisha wote na kila mmoja [mwenye mahusiano na
Somalia] analaanwa na kufanywa mhalifu, alisema. "Tunaitwa al-Shabaab kwa sababu
tu tumezaliwa Somalia. Tunatumai kuwa timu ya uchunguzi sio itabadlisha picha ya
hapa bali pia kuhakikisha usalama wetu."
Abdirizak Abdi, mwenye umri wa miaka 60, mzee
wa Eastleigh, aliiambia Sabahi kuwa jamii iko tayari kuisaidia timu ya
uchunguzi, lakini akasema kuwa serikali kwanza inapaswa kuwaelemisha watu juu ya
umuhimu wa kushirikiana na mashirika ya usalama.
Watu wengi wa eneo hilo wataachana na mchakato
huo ikiwa serikali itashindwa kuwahakikishia kuwa hawatakuwa wahanga wakati
watakapojitolea kutoa taarifa, alisema, na kuongeza kuwa watu walikataa kusaidia
uchunguzi kwa sababu polisi walikuwa wanamshughulikia kila Msomali kama
mshukiwa.
"Watu wanapaswa kuelemishwa juu ya kwa nini
wanahitaji kushirikiana na kuhakikishiwa usalama wao," Abdi alisema.
Post a Comment