Lionel
Messi
BARCELONA, Hispania
Hivyo Man City - ambao ni mabingwa wa England
na Chelsea waliovuliwa ubingwa wa Ulaya hivi karibu na kutupwa katika michuano
ya Europa League, zitapaswa kuvunja benki kama zinahitaji saini ya nyota huyo
anayevunja rekodi za soka kila uchao
KLABU mbili za Ligi Kuu ya England za Manchester
City au Chelsea zilizowahi kuripotiwa kuwania saini ya mshambuliaji Lionel
Messi, sasa zitalazimika kuvunja benki na kulipa dau la pauni milioni 312
kumpata.
Mwanasoka Bora huyo kwa mwaka wa tatu mfululizo
amekubakli kurefusha mkataba kwa miaka sita zaidi akiwa na klabu yake ya FC
Barcelona wenye thamani ya pauni milioni 17 kwa mwaka, unaofikia tamati mwaka
2018.
Mshahara huo unamfanya utamuwezesha kupata pauni
milioni 102 katika kipindi chake cha mkataba na Barca, ambapo ukijumlisha na
kipengele kinachomruhusu kuondoka klabuni Nou Camp kwa pauni milioni 210,
inamfanya Messi kuwa na thamani ya pauni milioni 312 kwa
sasa.
Hivyo Man City - ambao ni mabingwa wa England na
Chelsea waliovuliwa ubingwa wa Ulaya hivi karibu na kutupwa katika michuano ya
Europa League, zitapaswa kuvunja benki kama zinahitaji saini ya nyota huyo
anayevunja rekodi za soka kila uchao, huku akiwa na nafasi kuibwa kutwaa tuzo ya
nne ya Mwanasoka Bora wa Mawaka wa Fifa.
Ukiondoa kiwango cha pesa inayoweza kumuondoa
Messi katika soka la England, imeelezwa na inajulikana uwapo wa nafasi finyu ya
Messi, 25, kukubali kuihama Barca kuhamia klabu yoyote ya Ligi Kuu ya
England.
Kiungo nyota wa klabu hiyo na mhimili mkuu wa
mafanikio ya Barca, Xavi, 32, na nahodha mkongwe wa Carles Puyol, 34, nao pia
wamekubali kurefusha mikataba yao ya kuendelea kukipiga Nou
Camp.
Akizungumzia nyongeza za mikataba ya wakali hao,
Mkurugenzi wa Barca Toni Freixa alisema: “Puyol, Messi na Xavi ni nguzo tatu za
msingi. Ilikuwa jambo muhimu kuhakikisha tunabaki nao kwa kuwafunga na mikataba
mipya.
“Ni uamuzi uliokuwa na baraka zote za Bodi ya
Klabu, kufanya tulichofanya ili kuwabakisha Nou Camp ili kuendeleza programu
kutokana na nyongeza zao,” alisema Freixa.
Kabla ya mkataba mpya, Messi alikuwa akilipwa
mshahara wa pauni milioni 10 kwa mwaka, pamoja na asilimia 30 ambayo ilikuwa
ikijumuishwa kutokana na kiwango chake dimbani kupanda, lakini mkataba huu
utaigharimu zaidi na zaiodi Barca kutokana na sheria mpya za kodi za
hapa.
Post a Comment