Kilimanjaro Stars
The Uganda Cranes
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Tanzania Bara kukutana na Uganda katika hatua za mwisho za michuano hiyo baada ya kukutana mwaka 2010 katika fainali ambapo Tanzania ilishinda kwa penati 5-4 na kisha mwaka 2011 ambapo Uganda walishinda kwa 3-2.
Kwa maana hiyo Tanzania Bara inashuka uwanjani ikiwa na kila sababu na kiu ya kushinda sio tu ili kulipiza kisasi bali kuonyesha kwamba kinachosemekana kuwa kiwango chake kimepanda sio suala la kwenye vijiwe vya kahawa tu bali pia hata uwanjani.
Ili kufikia hatua hiyo ya nusu fainali, Uganda iliwatoa nishai Ethiopia kwa jumla ya goli 2-0 wakati Tanzania Bara iliwaengua Rwanda kwa jumla ya magoli hayo hayo 2-0.
Unaweza kutizama mechi hii Live Kuanzia saa Moja Jioni (7:00pm) Kupitia DStv’s Super Sport 9 East kutokea Namboole Stadium jijini Kampala.
Kabla ya Tanzania Bara kupambana na Uganda, timu ya Zanzibar(Zanzibar Heroes) watamenyana na timu ya Kenya (Harambee Stars) katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali utakaopigwa katika Uwanja wa Namboole. Unaweza kuutazama mchezo huu Live kupitia DStv’s Super Sport 9 East kuanzia saa kumi jioni(4.00pm).
Mechi hizi mbili zinamaanisha kwamba endapo Zanzibar wataifunga Kenya na baadae Kili Stars kuwatoa Uganda, timu za Tanzania ndizo zitakazokutana fainali. Je una ubashiri wowote kuhusu mechi hizi?Sema usikike.
Zanzibar Heroes
Harambee Stars
picha kwa hisani ya Mohammed Zubeiry
Post a Comment