Viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa wakiwa katika
mkutano wa maandalizi ya fainali ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania na Bodi ya
Miss Utalii Tanzania 2012/2013 zitakazofanyika hivi
karibuini
Bodi ya Miss Utalii Tanzania ikiwa
katika kikao cha pamoja na Viongozi wa Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA)
Wajumbe wa Bodi ya
Miss Utalii Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA).
****************
WAKATI kambi ya
Miss Utalii Tanzania 2012/2013 ikikaribia kuanza katika Hotel ya Ikondolelo
jijini Dar es salaam, juzi tarehe 14.12.2012 Bodi ya Taifa ya mashindano hayo
ilifanya kikao na Serikari kupitia Baraza la Sanaa la Taifa katika ukumbi wa
Baraza hilo. Katika kikao hicho ambacho kilijadili maandalizi ya fainali na
mpango mkakati wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka
huu.
Katika kikao hicho
Bodi ya Miss Utalii Tanzania iliwasilisha taarifa ya kukamilika kwa maandalizi
kwa Serikali ambapo bodi iliitaarifu Serikali kuwa maandalizi ya fainali hizo
yamekamilika kwa asilimia tisini 90% ikiwemo katika maeneo ya kambi na mafunzo,
ukumbi, Zawadi, wadhamini,Washiriki, Nk.
Bodi ilibainisha
kuwa kwamba jumla ya washiriki sitini (60) wakiwakilisha mikoa yote ya Tanzania
na Kanda maalum za vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii
Tanzania 2012/2013. Pia Bodi ilibainisha kuwa zawadi zitakazo tolewa kwa
washindi zimelenga zaidi kuwanufaisha washiriki , jamii zao na taifa. Zawadi
hizo ni pamoja na Nafasi za masomo za elimu ya juu, mikataba ya kazi ,Safari za
kushiriki mashindano ya Dunia na Kimataifa , Tuzo za heshima za kijamii,
kitalii, kitamaduni, urembo na mitindo.
Aidha Bodi
ilielezea kuwa imejipanga kuzifanya fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania
2012/2013 kuwa tukio kubwa la pekee Kihistoria na kitamaduni kuwahi kufanyika
nchini kabla na baada ya uhuru. Ambapo wakiwa kambini washiriki watafanya
shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kupata mafunzo stadi mbalimbali za
maisha , uhamasishaji na utangazaji wa elimu , utalii, utamaduni,
uwekezaji,mazingira, michezo na afya.
Nayo Serikali
ilipongeza Bodi ya maandilizi ya miss utalii Tanzania kwa mpango mkakati na
maandalizi yenye kukidhi na kulenga kupromoti utalii uhamasishaji na utangazaji
wa elimu, utamaduni, uwekezaji,mazingira, michezo na afya.Akizungumza katika
mkutano huo Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa
Ndugu.
Malimi Mashili
alipongeza mpangilio wa zawadi na tuzo kwa washindi pamoja na washiriki ambapo
tofauti na mashindano mengine ambapo zawadi zao huwa ni mzigo kwa washiriki na
wakati mwingine zisizo na manufaa kwa jamii wala Taifa."
Miss utalii
Tanzania katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni
fahari ya Taifa na kielelezo cha utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimafaifa
ambapo limekuwa ndilo shindano pekee linalo la tangaza nchi yetu kwa kushinda
mataji ya Dunia na kimataifa kila mnapo shiriki".
Aidha akiahirisha
mkutano huo aliihakikishia Bodi kuwa Serikali inatambua juhudi na mchango wa
waandaaji na mashindano ya miss utalii tanzania katika kukuza utalii, utamaduni
na michezo nchini na kwamba Serikali sikuzote ipo bega kwa bega na waandaaji wa
mashindano haya katika kuhakikisha kwamba hayakwami na iko tayari kusaidia kwa
hali na mali ili yaweze kufanyika kwa kiwango cha kimataifa.
Imetolewa
na,
Mratibu Matukio,
Hamis .A. Mkongowale
Post a Comment