Mke wa Rais na Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akikata utepe
ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya kwa vikundi vya
SACCOS vya UVIMA (Umoja wa vikundi vya WAMA Tawi la Majohe lililoko wilayani
Ilala) na Salma Kikwete SACCOS kilichoko Mkuranga. Uzinduzi huo ulifanyika
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012 na kuhudhuriwa pia na Waziri wa
Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi (wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina
(katikati) na kulia ni Afisa wa WAMA ndugu Tabu Likoko akifuatiwa na Grace
Michael, Afisa Habari wa Bima ya Afya.
Mwenyekiti wa WAMA Mama
Salma Kikwete na viongozi wengine wakiangalia moja ya kadi ya mwanachama wa bima
ya Afya mara tu baada ya kuzindua rasmi huduma ya bima hiyo kwa wajasiriamali wa
UVIMA na Salma Kikwete SACCOS kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.
Wengine katika picha kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Mheshimiwa Dr. Husein Mwinyi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mheshimiwa
Deogratias Ntukamazina na Mkurugenzi wa Mfuko huo Ndugu Emmanuel
Humba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko
wa Bima ya Afya kwa Bibi Tatu Ngao, Mwenyekiti wa UVIMA mara tu baada ya
kuzindua rasmi mpango huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe
20.12.2012.
Waziri wa Afya Mheshimiwa
Dr. Hussein Mwinyi akimpatia tuzo ya Shujaa wa mfuko wa Bima ya Afya kwa mwaka
2012 Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa WAMA kwa jitihada zake kubwa za kumkomboa
mwanamke kiuchumi na kijamii na pia katika kupigania afya kwa wote na hasa
makundi maalum katika jamii. Tuzo hiyo ilitolewa baada ya uzinduzi wa huduma ya
Bima ya Afya kwa vikundi vya wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS
uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012. PICHA NA JOHN
LUKUWI.
Post a Comment