Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mussa Kitale aendeleza dua kwa Sharomillionea

 

Mussa Kitale kulia akiwa na swahiba wake, marehemu Sharomillionea
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa vichekesho na swahiba wa marehemu Hussein Mkiety, maarufu kama 'Sharomillionea', Mussa Kitale, ameendelea kumlilia nyota huyo kwa kusema haamini kama ni kweli siku zimekwisha na sasa wanasubiria kumfanyia dua arobaini kipenzi chao, kama anavyofanya kumuombea dua kila mara.
Huu ni Mussa Kitale, Rais wa Mateja
Sharomillionea alibambwa maeneo ya jiji la Dar es Salaam, akizungumza na wenzake juu ya kukaribia kwa arobaini ya Sharomillionea inayotarajiwa kusomwa kijijini kwao Lusanga, Januari nne mwaka huu.

"Kweli siku zinakimbia jamani, yani tayari tunakwenda kuhitimisha kabisa maisha ya duniani ya mwenzetu Sharomillionea? Hii ni hatari na hakika Mungu amlaze mahali pema peponi mpiganaji wetu Mkiety.

"Arobaini yake itafanyika kijijini kwao Lusanga ikionyesha kuwa katika kipindi hiki tulikuwa wapweke kwa kukosa uwepo wa Sharomillionea,” alisema Kitale ambaye pia ni mwimbaji wa Bongo Fleva, akitamba na wimbo wa ‘Hili dude Noma’.

Sharomillionea alikuwa na ukaribu wa kupitiliza na Kitale, kwani inadaiwa hata siku aliyopata ajali Tanga, alikuwa aking’ang’ania kusafiri na Kitale aliyekuwa njiani kutoka Iringa kwenye shoo na marehemu alikuwa akielekea Tanga.

Mbali na hilo, pia wasanii hao wamekuwa pamoja kila wakati na kufanya kazi pamoja, hasa baadhi ya nyimbo walizochanganya sauti au video zao, bila kusahau filamu za vichekesho walizokuwa pamoja, ikiwamo Mtoto wa Mama, Vituko Show zote, Jini Mahaba, Porojo na nyinginezo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top