(picha credit: Blogu ya
Mhe. Dkt. F. Ndugulile Mbunge wa Kigamboni, CCM)
Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) litaanza kuziuza nyumba zake zinazojegwa katika eneo la Kibada katikati ya
wiki hii.
NHC iemesema nyumba zake
216 zinazojengwa katika maeneo hayo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam,
hazitauzwa kwa zaidi ya Shilingi milioni 50, ili kumwezesha mwananchi wa kawaida
kuzinunu.
Taarifa hiyo ilitolewa jana
na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mikoa na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, wakati
wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea miradi ya ujenzi wa
nyumba za shirika hilo.
“Kigamboni pale Kibada tuna
nyumba za aina mbili, yaani zipo za vyumba viwili na nyingine za vyumba vitatu.
Kwa kuwa lengo letu siyo kupata faida bali ni kuwasaidia wananchi ili waweze
kumiliki nyumba badala ya kuendelea kupanga, nyumba hizo zitakapoanza kuuzwa
hazitauzwa kwa zaidi ya Sh milioni 50. Pamoja na kwamba lengo letu ni hilo, bado
tunaiomba Serikali iondoe VAT kwa vifaa vya ujenzi ili nyumba ziweze kuuzwa kwa
bei ya chini zaidi,” alisema Mndolwa.
Naye, mmiliki wa Kampuni ya
Shibat Enterprises Limited, Edwin Shitindi ambayo imepewa tenda ya kujenga
nyumba 104 katika eneo hilo la Kigamboni, alisema atahakikisha nyumba hizo
zinakamilika ndani ya miezi mitano kuanzia sasa. Alisema kampuni yake
itajitahidi kuzijenga katika ubora unaotakiwa kwa kuwa zitakapoanza kutumika
zitatumiwa na Watanzania.
Wadau ambao wana nia ya
kumiliki nyumba kwenye eneo hilo wanashauriwa kutembelea tovuti ya NHC (www.nhctz.com) kuanzia Jumatano ya wiki
hii ili kupata maelezo zaidi juu ya bei, ulipaji na umiliki wa nyumba
hizo.
Post a Comment