Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, D. A.
MISIME – ACP.
JESHI la
Polisi Mkoa wa Dodoma, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kujihusisha na
shughuli za wizi wa mtandao hususani katika maduka yanayotoa huduma za
M-PESA,Tigo Pesa na Airtel Money katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya
Dodoma.
Watu hao
ambao wanadaiwa kujipatia zaidi ya shilingi 1,730,000 /= kwa Mawakala wanne
tofauti wanaotoa huduma hizo walikamatwa jana tarehe 19/12/2012 majira ya saa
12:00 hrs mchana.
Watuhumiwa hao ambao wanatokea Jijini Dar es
Salaam majina yao ni Mohamed s/o Dotto @ Sefu, mwenye umri wa miaka (30)
Mnyamwezi mkazi wa Kigogo, Mohamed s/o Pazi, Mzaramo Miaka (28)
na Ally s/o Mohamed miaka (25) ambao ni wakazi wa
Ilala.
Wamekuwa
wakitumia mbinu mbalimbali kufanikisha wizi huo, moja ya mbinu ni kwenda kwenye
maduka yanayotoa huduma hizo na kumwambia wakala kuwa wanaharaka
na kutaka kuweka Pesa kiasi fulani ambacho wanakuwa nazo mkononi na
kuanza kuzihesabu.
Mara
meseji ya pesa toka kwa wakala zinapoingia katika simu zao, simu zao huita
wakati huo huo na kujifanya wanapokea simu huku
wakisogea pembeni wakiongea na simu na kuondoka julma kwenda kuzitoa mahala
pengine kwa haraka.
Wakala
walioathirika na Wezi hao mpaka sasa ni Consolata d/o Martini ambaye duka lake
liko eneo la Kuu Streetu shilingi 300,000/=, Perndo d/o Martin qambaye Duka lake
liko eneo la CBE Tsh. 860,000/= Mlay s/o Felix eneo la Makole Tsh. 300,000/=,
Masala s/o Mabula wa eneo la Changombe Tsh. 70,000/= na Duka la Lazia Shop
ambalo liko Mtendeni Street Tshs 200,000/=.
Natoa
wito kwa wamiliki na wakala wote wanatoa huduma hizo kuwa makini wanapoendesha
shuguli zao, kwa kutoa taarifa za watu wanaowatilia shaka wanaofika kutaka
huduma katika maduka yao mara moja ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
[D. A. MISIME –
ACP]
KAMANDA WA POLISI [M]
DODOMA
CONTACT:
POLISI
MKOA WA DODOMA
DAWATI LA
HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone: 0715 006523 – Luppy Kung’alo –
Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone: 0712 360203 –
Silyvester Onesmo – Police Konstebo
(PC)
Post a Comment