Kutoka LINDI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Jakaya M. Kikwete yupo katika ziara ya kikazi
Mkoani Lindi ambapo amehudhuria Maazimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo
kitaifa yamefanyika Mkoani hapa na pia anakagua na kufuatilia mipango na miradi
mbalimbali ya Maendeleo.
Miongoni mwa Miradi aliyozindua ni pamoja na
Daharia ya Shule ya Wanawake Nachingwea iliyopo eneo la Bomani wilayani
Nachingwea. Shule hiyo maaalum ya Wanawake imejengwa kwa nguvu za Wananchi wa
Nachingwea wenyewe kwa kuchangishana kwa kushirikiana na Serikali.
Ujenzi wa Shule hiyo ulianza 2010 kutoka katika
ruzuku ya Serikali katika mpango wa Serikali kuwainua na kuwawezesha wanawake
kwa kuwapa fursa za Elimu kwa kuangalia namna ya kukabiliana na Changamoto
zinazowakabili watoto wa kike, kama mimba za utotoni,umbali na mkakati wa
kuongeza idadi ya watoto wa kike mashuleni.
Mheshimiwa Rais alitoa msaada wa pesa
taslimu na ahadi ya kujenga Maabara, Viwanja vya michezo, Uzio, Jengo la
Utawala, Bweni na Kuongeza Idadi ya Walimu. Pia aliipongeza Halmashauri ya
wilaya hiyo kwa kupata wazo la kuendeleza majengo yaliyoachwa magofu kwa
kutengeneza Shule hiyo.
Baada ya Uzinduzi huo Mheshimiwa aliendelea
na ratiba yake ya kuhudhuria na kufanya Uzinduzi wa Miradi mbali mbali ya
Maendeleo katika maeneo mengine ya Mkoa wa Lindi.
Post a Comment